Friday, January 31, 2014

Mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara wawasili leo mjini Musoma Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa akiongoza waombolezaji
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema  wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.

Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.

No comments:

Post a Comment