Thursday, January 23, 2014

kilomita 1552.18 za barabara zajengwa mkoani mara kati ya septemba na desemba 2013 KIKAO CHA BODI YA BARABARA
 
Meneja wa Tanroads mkoa wa mara Emanuel Koroso akizungumzia hali ya barabara
                                    Injinia Emanuel Koroso

 mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara mkoa wa mara ambaye ni mkuu wa mkoa wa mara john tuppa akiongoza kikao
Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vicenti Nyerere katikati nae alikuwepo
 Mbunge Wa Jimbo La Musoma Vijijini Nimrod Mkoano Akichangia Masuala Ya Barabara
Mkuu wa Uhamiaji Mara akiwa katika kikao
SERIKALI imetenga jumla ya shilingi bilioni 12.7 bajeti ya matengenezo mbalimbali ya barabara na madaraja mkoani Mara kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo jumla ya kilomita 1552.18 za  barabara na madaraja 60 yalifanyiwa ukarabati kuanzia septemba hadi desemba mwaka jana.

Hayo yameelezwa jana na meneja wakala wa barabara TANROADS mkoani hapa Eng. Emmanuel Korroso wakati anawasilisha taarifa ya utekelezaji na mapendekezo ya bajeti,matengenezo sambamba na miradi ya maendeleo kwenye kikao cha wajumbe wa bodi ya barabara kilichofanyika ukumbi wa uwekezaji ofisiya mkuu wa mkoa huo.

Alisema serikali pia imetenga  shilingi 2,144.87 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye barabara mbalimbali na kwamba kilomita 2.2 zitajengwa kwa kiwango cha lami huku kilomita 45.5 zitakarabatiwa kwa changarawe katika wilaya mbalimbali za mkoa huo.

‘’Jumla ya fedha iliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ni shilingi 14.9 milioni kwa ajili ya kazi ya matengenezo na kazi za miradi ya maendeleo ambapo fedha hizi ni ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2012/2013’’alisema Korroso na kuongeza.  

 ‘’hadi kufikia mwisho wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2013/2014 utekelezaji wa kazi za matengenezo ulikuwa umefikia asilimia 66.’’

Akizungumzia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kitaifa meneja huyo wa wakala wa barabara mkoani humo alisema kuwa serikali imetumia bilioni 85.363 kwenye ujenzi wa barabara kuu itokayo mkoani Simiyu hadi manispaa ya wilaya ya Musoma mjini mkoani hapa.

Kilomita 74 kati ya kilomita 85.5 zimekamilika ukarabati huu pia unahusisha ujenzi wa madaraja mawili makubwa ya Rubana na Suguti ambayo tayari yamekamilika’’ aliongeza.

Hata hivyo alisema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya kichina ya M/s Chiko chini ya mhandisi mshauri wa mradi huo ambao ni Consulting Engineering Services (India) Private ltd ikishirikiana naNorplan(T) ltd kampuni ya kizalendo.

No comments:

Post a Comment