Friday, December 20, 2013

RAIS KIKWETE ATENGUA UTEUZI WA MAWAZIRI WAKE WANNE NI KATIKA SAKATA LA OPARESHENI TOKOMEZA UJANGILI


Rais Jakaya Kikwete ametengua rasmi uteuzi wa Mawaziri wa nne waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za kiraia wakati wa Oparesheni Tokomeza Ujangili iliyokuwa ikiendeshwa na Serikali.
Akisoma Bungeni mjini Dodoma leo jioni, Taarifa hiyo ya Rais, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Bungeni mjini Dodoma kuwa Rais ameridhia maoni ya Wabunge wakati wa kujadili ripoti ya Kamati iliyoundwa na kuongozwa na Mbunge James Lembeli kuwa Mawaziri waliotuhumiwa waondoke.
Mawaziri waliotakiwa kujiuzulu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Hamisi Kagasheki, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. John Nchimbi pamoja na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo.

Lakini kabla ya kutanga taarifa hiyo Bungeni Waziri Kagasheki alitangaza rasmi kujiuzulu mbele ya Spika na Bunge.
Aidha Wabunge pia walimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda naye kujiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia mawaziri wake. 

Kuenguliwa kwa Mawaziri hao kumekuja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe  James Lembeli kuwasilisha ripiti ya kamati yake na kujadiliwa kwa kina Bungeni hii leo.
Lembeli amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika. 

Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa  Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama.
Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugaji wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.

Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.

Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu  waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha.

No comments:

Post a Comment