Friday, December 6, 2013

Afrika Mashariki yaomboleza Mandela


Rais Kikwete ametangaza siku tatu za kuomboleza kifo cha Mandela,Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ametangaza siku tatu za maombolezi, kufuatia kifo cha mzee Nelsomn Mandela, akisema kua Afrika na dunia nzima kwa ujumla imempoteza shujaa mkubwa sana katika karne ya 20 na 21.

Kikwete alisema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kua Mandela ni kiongozi wa kipekee na mtu aliyeenziwa sana na dunia nzima pamoja na watu wa Afrika Kusini baada ya kupigania sana demokrasia nchini Afrika Kusini.
Kikwete alisema mfano wa Mandela unapaswa kuigwa na watu wote dunian,Kwa upande wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesema kuwa Mandela alikuwa mfano mzuri wa umuhimu wa kuwa na matumaini na kuwataka watu kuwa na uelewa wa kuwasamehe bila masharti wale wote wanaotukuosea.

Naye Rais wa Rwanda Paul Kagame,amesema kua Mandela ataendelea kuishi kwenye mioyo ya wengi wetu.

Naye Rais mstaafu Daniel Moi ambaye alikuwa madarakani wakati Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amempongeza Mandela kwa kuhakikisha utulivu wa kisiasa barani Afrika na kuwa mfano bora kwa viongozi wengine.

No comments:

Post a Comment