Saturday, September 28, 2013

NDUGU WAUA NA KUJERUHIANA KWA DENI LA SH,20,000


Serengeti:DENI la sh.20.000 limesababisha ndugu  watatu wa kitongoji cha Nyasuma kijiji cha Borenga kata ya Kisaka wilaya ya Serengeti kukatana mapanga na mmoja kufariki huku wawili wakilazwa katika hospitali teule ya Nyerere ddh chini ya  ulinzi wakiwa na hali mbaya.
 
Tukio hilo la aina yakelinadaiwa kutokea septemba 23 majira ya saa 12:00 jioni nyumbani kwa Muhochi Hacheri limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali teule ya Nyerere ddh,na kumtaja aliyefariki kuwa ni Julius Mwikwabe (20)aliyefariki,na majeruhi hao kuwa ni Mwikwabe Mwikwabe(40)Magubo Mwikwabe(29).
 
Magubo ambaye ni mtuhumiwa akiwa amelazwa kitanda namba 8 na kaka yake wakiuguza majeraha alisema ,alikuwa akimdai mdogo ambaye ni marehemu  sh,20,000 baada ya kumuuzia baiskeli aina ya Swala kwa sh,40,000 na kulipa nusu ,alipomdai ndipo kukaibuka ugomvi na kusababisha kifo na majeruhi kwao .
 
“Toka mwezi mei namdai pesa hizo akawa mkaidi…septemba 19 nilikwenda kudai akaahidi kesho yake angelipa  hakulipa…septemba 23 tulipokutana akanitolea majibu mabaya…nilimchapa fimbo nne kama mdogo wangu…akatoka kimya akaenda kunoa panga na jioni akaja nikiwa kwa Hacheri na kufika na kunikata kwa panga mgongoni chini ya bega la kushoto”alisema majeruhi huyo.
 
Alisema ndipo naye akachukua panga alilokuwa nalo kwa nia ya kujihami,lakini mdogo wake huyo ambaye ni marehemu alinyanyua panga amkate tena,”aliponyanyua mkono anikate nikamkata mkono wa kushoto ukaning’inia na damu zikawa zinavuja sana..alifariki baada ya kufika hospitalini”alisema.
 
Naye Mwikwabe Mwikwabe kaka mkubwa wa familia hiyo alisema ,akiwa nyumbani kwake alipata taarifa ya ugomvi wa wadogo zake ,”lengo likiwa ni kuwaamua…nikiwa katika pilika pilika hizo Julius(marehemu)alinikata sehemu ya bega la kushoto kwa nyuma huku akidai ni bahati mbaya,”alibainisha.
 
Alisema kitendo cha kukatwa kilimfanya aanze kujihudumia huku wadogo zake wakiendelea kupambana na matokeo ya ugomvi huo wamempoteza mdogo wao.
 
Muuguzi wa zamu wodi ya wanaume Hellen Mosha alisema kuwa Julius alifariki muda mfupi kabla ya kupata matibabu na chanzo kikiwa ni kuvuja damu sana kutokana na kuchelewa  kufikishwa hospitalini.
 
Polisi wilayani hapa wamesema watuhumiwa hao wawili wanatibiwa wakiwa chini ya ulinzi wakati uchunguzi zaidi ukiendelea wa kubaini mhusika aweze kufikishwa  mahakamania.
Mwisho. 
MWIKWABE MWIKABE NA MASUBO MWIKWABE AMBAO NI MTU NA MDOGO WAKE WAKAZI WA KIJIJI CHA BORENGA KATA YA KISAKA WILAYANI SERENGETI WAKIWA WAMELAZWA WODI LA WANAUME KITANDA NAMBA 8 HOSPITALI TEULE YA NYERERE DDH KUFUATIA UGOMVI BAINA YAO ULISABABISHWA NA DENI LA SH.20.000 NA KUPELEKEA MDOGO WAO JULIUS MWIKWABE KUFARIKI .


 WAMELAZWA WAKIWA WAMEFUNGWA PINGU KUTOKANA NA TUHUMA ZA MAUAJI YA MDOGO WAO

No comments:

Post a Comment