Wednesday, June 5, 2013

KWAHERI MANGWEA a.k.a MIMI

Sasa ni mda wa kuanza kutoa heshima ya mwisho kwa ndugu yetu Albert Mangweha hapa Leaders Club

Zoezi la kumuaga mwanamuziki wa kizazi kipya, Albert Keneth Mangwea ndio unaoendelea kwa sasa katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Baada ya zoezi hili waombolezaji wataanza msafara wa kuelekea Kihonda Morogoro ambako ndipo mwanamuziki huyo aliyethibitika kuwa kipenzi cha wengi atakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Umati mkubwa wa watu wanaonekana wakimiminika katika viwanja hivyo kumuaga.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amen

Gari lenye Mwili wa Marehemu Albert Mangwea
usalama wa kutosha
Umati wa watu waliohudhuria
Vijana wakiimba kwa huzuni kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea
credits: Lukaza & Mdimu blogs
Dah this is it ndugu yetu mpendendwa ndo ametangulia mbele za haki na sasa ule muda wa kutoa heshima za mwisho ndo umewadia. Mungu awape nguvu wale wote waliofikwa na msiba huu. Image credit DJ Choka

Mwili wa marhemu Albert Mangwea ukiwa kwenye jeneza tayari kwa watu kutoa heshima za mwisho

Umati wa watu wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kwenda kuaga huku kikosi cha msalaba mwekundu na polisi kikiwa stand by just incase anything happens. Sasa naskia watu badala ya kwenda na kuaga wao wako busy wanapiga picha kha hizi teknolojia aiseee tutajutaaaa 
Baadhi ya ma super star wa bongo wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuaga.

No comments:

Post a Comment