Chama cha
demokrasia na maendeleo CHADEMA kimesema kitendo cha serikali kupitia Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, uratibu na Bunge Mh. William Lukuvi bungeni
jana, kutangaza dau la Shilingi Mil 100 kwa yeyote atakayefichua taarifa za
tukio la kihalifu lililotokea Arusha mwishoni mwa wiki si la kiungwana.
Akizungumza
na
waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini
Dar Es
Salaam, Mkurugenzi wa habari na mawasiliano Mh. John Mnyika amesema
kitendo cha
serikali kutangaza dau hilo la shilingi mil. 100 ni utumiaji mbaya wa
rasilimali za Taifa na kuitaka serikali kutumia pesa hizo kwa kusaidia
famili za watu waliopoteza maisha bila hatia katika matukio mbalimbali
akitolea mfano wa familia ya aliyekuwa mwandishi wa habari, marehemu
Daud Mwangosi.
Akizungumzia
kauli iliyotolewa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mwenyekiti wa
chadema Mh. Feeman Mbowe, Mh. Mnyika amesema chama kimetoa Baraka zote kwa
mwenyekiti huyo kutokana na kauli hiyo na kuanzia sasa Wabunge wote wa Chadema
hawatoshiriki na hawaruhusiwi kushiriki vikao vya Bunge vinavyoendelea mpaka
hapo taratibu za maombolezo zitakapokamilika.
Aidha Mh.
Mnyika ameongeza kuwa chadema haijafurahishwa na kitendo cha Bunge kutositisha
shughuli zake kutokana na tatizo la Arusha wakati majanga mengine kama hayo yanapotokea
Bunge husitisha shughuli zake na taratibu zingine hufuata.
Wakati
huo huo MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mh.
Freeman Mbowe amefichua siri kuhusu tukio la mlipuko wa bomu lililotokea
jusi katika viwanja vya Soweto, jijini Arusha.
Katika
kauli yake jana, Mbowe ameibua tuhuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi,
ambapo alidai kuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ndiye
aliyerusha bomu hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa,baada ya kutembelea majeruhi katika
Hospitali ya Selian, Mbowe alisema chama chake kina ushahidi wa kutosha
juu ya askari huyo kurusha bomu.
Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa
kambi ya upinzani bungeni,alisema wamefanikiwa kupata ushahidi wa
kutosha juu ya tukio hilo baya linalochafua taswira ya nchi.
Alisema chama chake kipo tayari kuweka ushahidi huo hadharani, iwapo Serikali itaendelea kufanya siasa na kuficha ukweli.
|
No comments:
Post a Comment