
Wabunge
wa Chadema, Mh Lema, Mh John Mnyika, Mh Mashishanga, Mh Tundu Lissu na
Grace Kiwhelu wakiwa wamebeba jenenza leneye mwili wa marehemu Judith
William Moshi kuelekea makaburi ya Sokoni 1 kwa maziko. Marehemu Judith
alifikwa na mauti baada ya kulipukiwa na bomu siku ya Mkutano wa Chadema
kuhitimisha kampeni zake kwa udiwani wa Kata ya Kaloleni, mkutano
uliofanyika uwanja wa Soweto siku ya Jumamosi Juni 15, 2013. Wabunge
wengi wa Chadema walishiriki ibada na kuhudhuria mazishi wakiongozwa na
mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Freeman Mbowe.

Misa katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Sokon 1

Msafara
wa kwenda Makaburini ukiongozwa na Askofu Isaac Kasir katka Kanisa la
KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Sokoni 1

Baadhi ya wabunge wa Chadema wakiwa na huzuni eneo la makaburi

Jeneza likiteremshwa kaburini

Ndugu wa marehemu

Wabunge wa Chadema

Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” wakiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu

Mtoto wa marehemu akilia kwa uchungu sana baada ya kuweka shada la maua. Marehemu Judith ameacha watoto watatu wote wa kike

Msafara
wa wafuasi wa Chadema ukitoka Hospitali ya Mt Meru kuelekea Kata ya
Sokoni 1 ambako ndipo misa ya kumuombea marehemu na maziko ya Judith
Moshi aliyekufa kwakulipuliwa na bomu Jumamosi iliyopita ilifanyika

Msafara ukikatiaza mitaa ya Jiji kiasi cha kusimamisha shughuli zote katika njia ilikopitia

Mbunge wa Ubungo, Mh John Mnyika akisalimiana na wachungaji baada ya mazishi

Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na mkewe wakienda kuweka shada la maua

Wabunge kina mama nao wakiweka mashada ya maua

Wananchi wa kawaida nao wakishiriki kuweka mashada ya maua

Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni Mh Tundu Lissu akiweka shada la maua

Viongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha

Viongozi wa Chadema Wilaya. Picha zote na Tumainiel Seria
Hapa ni Sugu akiwa na Peter Msigwa wakiongoza msafara.
Hili ndilo jeneza lililolobeba mwili wa marehemu ukipelekwa Sokon 1

Vijana
walioko kwenye mafunzo ya upolisi wakiwa juu ya kanisa linaloendelea
kujengwa wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Judith William Moshi.
Chadema inawatuhumu Polisi ndio waliolipua bomu na kupiga risasi
zilizoua 4 na kujeruhi zaidi ya 67 katika mkutano wake
No comments:
Post a Comment