Monday, May 6, 2013

UTOAJI MIMBA UKOMESHWE NCHINI TANZANIA!!

Wadau wa masuala ya sheria nchini Tanzania wametakiwa kuweka utaratibu wa kisheria ambao utasaidia kuzuia vitendo vya utoaji mimba tofauti na taratibu zilizopo hivi sasa ambazo zinaonekana kushindwa.

Mwanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake nchini Tanzania TAWLA Bi. Anna Marie amesema hayo wakati akitoa mada kwa wanahabari juu ya tatizo la utoaji mimba ambalo hivi sasa linaonekana kushamiri nchini.

Bi. Marie amesema licha ya kuwepo kwa sheria ya kuzuia utoaji mimba, sheria hiyo imekuwa kama haifanyi kazi kutokana na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na vitendo vyenyewe kufanyika katika mazingira ya siri.

No comments:

Post a Comment