Friday, May 24, 2013

TAKUKURU YAMFIKISHA MAHAKAMNI KATIBU TAWALA MSTAAFU MARANa Shomar Binda

Musoma
 
TAASISI ya Kuzui na Kupambana na Rushwa mkoani Mara (TAKUKURU) imemfungulia Shauri la jinai namba 85 ya mwaka 2013 inayohusu matumizi mabaya ya mamlaka aliyekuwa Katibu Twala wa mkoa wa Mara Clement Lujaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoni humo.
 
Mashitaka hayo ya matumizi mabaya ya mamlaka yamefikishwa Mahakamani mbele ya Hakimu Janety Musalocha na Mwendesha mashitaka wa Takukuru Elick Kiwia.

Akitoa ufafanuzi wa mashitaka hayo,Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mara Holle Makungu amewaeleza Waandishi wa Habari kati ya tarehe 15 februari 2010 na julai 2011 Katibu Tawala huyo kwa kutumia wadhifa wake kama Afisa Masuhuri wa mkoa wa Mara kwa nyakati tofauti katika kipindi hicho alidhiinisha magari ya Serikali yaliyo chini ya usimamizi wake yafanyiwe matengenezo katika karakana (garage) za watu binafsi pasipo kukaguliwa.

Alisema kutokana na utaratibu uliopo,magari yote ya Serikali yanatakiwa kupata kibali cha matengenezo kutoka kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) hivyo kitendo cha Katibu Tawala huyo kupeleka katika karakana za watu binafsi ni kinyume cha utaratibu.

Mkuu huyo wa Takukuru alieleza kuwa kutokana na kitendo hicho kulipelekea watu binafsi kujipatia faida bila ya uhalali jumla ya kiasi cha shilingi milioni kumi na nane,laki nane, therathini na sita elfu,mia nane na tano (18,836805/= kitendo ambacho ni matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa bila ya mshitakiwa kuwepo Mahakamani kwa kuwa hayupo Mjini Musoma imepangwa kutajwa tena Mahakamani hapo juni 18 ambapo mshitakiwa ametakiwa kuwepo siku hiyo ili aweze kujibu shitaka linalo mkabili.

Hakimu Musaroche ametoa hati ya wito kwa mshatakiwa chini ya kifungu cha 100 cha Sheria ya Mwenendo wa Mkosa ya Jinai,Sheria namba 20 kama ilivyofanyiwa Mapitio mwaka 2002 inayomtaka mshitakiwa kufika katika Mahakama hiyo tarehe tarehe 18/6/2013.

Takukuru mkoa wa Mara imewataka maafisa masuhuri katika Mamlaka za Umma ikiwa ni pamoja na makatibu Tawala wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halimashauri,Wakala wa Serikali ambao wana mtindo wa kutengeneza magari ya Umma katika karakana za watu binafsi bila kufuata utaratibu sahihi wa kisheria wa matengenezo ya magari ya Serikali kuacha kufanya hivyo.

Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Mara alisema ofisi yake italazimika kuanzisha uchunguzi dhidi ya maafisa masuhuri ambao wanafanya vitendo hivyo ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

No comments:

Post a Comment