Thursday, May 30, 2013

TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI - 29.05.2013: 
MAUAJI:
Mnamo tarehe 28.05.2013 majira ya saa 16:00 hrs. huko maeneo ya Kwangwa, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara; ESTER D/O ELIAS, miaka 15, Mkabwa, Mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari ya Kamunyonge amekutwa amekufa katika kichaka kilichopo karibu na nyumbani kwao huku akiwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye shavu la kulia pia alichomwa na kitu cha ncha kali kwenye paja la kushoto.

Uchunguzi wa tukio hili unafanyika kwa kina ili kubaini chanzo cha mauaji haya. Watuhumiwa wawili (2) wamekamatwa ambao ni: JUMA S/O HUSSEIN, miaka 34, mkazi wa Nyakato na MAKUNDI S/O MWITA, miaka 34, mkazi wa Nyakato. Wote wanahojiwa kuhusiana na tukio hili.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara; Anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa za siri juu ya mauaji haya wazitoe kwa katika vyombo vya dola.


ABSALOM A. MWAKYOMA - SACP.
KAMANDA WA POLISI MKOA MARA - MUSOMA.

No comments:

Post a Comment