Wednesday, May 15, 2013

MWAKALEBELA MFANO WA KUIGWA, KITABU CHAKE HADHARANI MEI 18 TAIFA!!

1


Na Mwandishi Wetu
 
KITABU cha kwanza nchini kinachozungumzia soka la Tanzania kijulikanacho kwa jina la “Soka la Tanzania” kitaanza kuuzwa siku ya mechi ya watani wa Jadi, Yanga na Simba iliyopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.
 
Akizungumza na jijini jana, mtunzi wa kitabu hicho, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na yamedhaminiwa  na kampuni TSN Group kupitia kinywaji chake cha kuongeza nguvu Chilly Willy, Events World, Vannedrick Tanzania Limited na  Inbox Pub.
 
Wadhamini wengine ni Clouds FM, Times FM na Street Soul kwa mujibu wa Mwakalebela. Alisema kuwa kwa sasa ametoa nakala 10,000 kwa ajili ya kuuzwa Tanzania nzima. Alisema kuwa kitabu hicho kimezungumzia historia ya soka la Tanzania katika Nyanja za vijana, wanawake na wanaume, ligi kuu ya Tanzania Bara, Taifa Cup, Timu ya Taifa na Utawala Bora.
Mbali ya hayo, kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo, mchango wa serikali katika kuinua mpira wa miguu, wadhamini, uhusiano kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu Tanzania.
 
“Pia nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi cha miaka mine nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa kwanza  Juni 15, 2006,” alisema Mwakalebela.
 
Alisema kuwa kitabu hichi ni muhimu sana kwa wana-habari, wachezaji, makocha, waamuzi na wadau wengine wa mchezo huo kwani kuna kumbukumbu zote za mechi za timu ya Taifa ikiwa mabao ya kufunga, wafungaji, vikosi tofauti vya timu za taifa na mambo mengine.

No comments:

Post a Comment