Thursday, May 16, 2013

Chelsea imekuwa Timu ya kwanza toka Uingereza kuweka historia ya Kubeba UEFA CHAMPIONS LEAGUE na EUROPA LEAGUE Mfululizo.


HISTORIA:Chelsea becomes the first English team to win all three major European Club competitions, having already claimed the Champions League and the (defunct) Cup Winner’s Cup!


Shujaa wa Mechi hii ni Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, ambae Mwaka jana hakucheza Fainali ya Kombe la Europa League kwa kuwa Kifungoni, kwa kufunga Bao la Pili na la ushindi kwa kichwa katika Dakika ya 92.
 


Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0 huku Benfica wakionyesha umilikaji mpira wa hali ya juu lakini staili yao ya uchezaji ya kutaka ‘kutembea’ na mpira hadi wavuni ndio iliwaangusha.



HISTORIA:Chelsea becomes the first English team to win all three major European Club competitions, having already claimed the Champions League and the (defunct) Cup Winner’s Cup!



Goli la mchezaji  Branislav Ivanovic dakika ya pili ya muda wa nyongeza kati ya tatu baada ya kutimu dakika 90 za kawaida kumalizika , hapo jana (May 15,2013) limeipa Cheslea Kombe la Europa League baada ya kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena nchini Uholanzi.

Beki huyo wa Serbia, alipaa hewani kwenda kuufuata mpira wa kona uliopigwa na  Juan Mata na kuujaza nyavuni.


Shujaa wa Mechi hii ni Beki wa Serbia, wa Chelsea  Branislav Ivanovic, ambae Mwaka jana hakucheza Fainali ya Kombe la Europa League kwa kuwa Kifungoni, kwa kufunga Bao la Pili na la ushindi kwa kichwa katika Dakika ya 92.


Branislav Ivanovic akipongezwa na hapo jana(May 15,2013 katika fainali ya Kombe la Europa League baada ya Chelsea kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.


Torres akimpiga chenga kipa wa Benfica kabla ya kufunga bao la kwanza kwa Chelsea hapo jana(May 15,2013 katika fainali ya Kombe la Europa League baada ya Chelsea  kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.



Gwiji Patrick Kluivert akiwasilisha Kombe la Europa uwanjani hapo jana(May 15,2013 katika fainali ya Kombe la Europa League baada ya Chelsea kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.



Bango:Likisema’’Tunamtaka Mourinho: Mashabiki wa Chelsea waliwasilisha hisia zao pia  juu ya kocha atakayerithi mikoba Rafa Benitez ‘’ hapo jana(May 15,2013 katika fainali ya Kombe la Europa League baada ya Chelsea  kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.

Ile balaa ya Benfica kutotwaa Taji lolote Ulaya kwa Miaka 51 tangu enzi za Nguli wao Eusebio, licha ya kutinga Fainali 7 sasa, linazidi kuendelea.


Rodrigo wa Benfica na Cesar Azpilicueta wa Chelsea.
Wapo Mashabiki wa Benfica wanaoamini kuwa hiyo ni laana toka kwa aliekuwa Kocha wao, Bela Guttmann, ambae ndie aliwapa Taji lao la mwisho Mwaka 1962 wakati Eusebio akichaza walipoicharaza Real Madrid Bao 5-3 na kuwa Mabingwa wa Ulaya.
Baada ya hapo, Bela Guttmann aliondoka Benfica kwa mzozo na kuapa na kulaani kuwa Benfica haiwezi kutwaa tena Taji la Ulaya bila ya yeye.

Kwa bahati mbaya, Bela Guttmann ni marehemu na licha ya Mashabiki wengi wa Benfica kupeleka Maua Kaburini kwake na kuomba laana iondoke inaelekea mambo hayajatengemaa.

No comments:

Post a Comment