Monday, May 13, 2013

BUNDUKI NNE ZINAZOTUMIKA KATIKA UHALIFU ZAKAMATWA MKOANI MARA

Na Shomari Binda
     Musoma


JESHI la polisi mkoani Mara limekamata bunduki nne zinazodaiwa kutumika katika matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yamekuwa yakilipotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kupelekea watu kudhuliwa na kunyang'anywa mali.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari juu ya utekelezaji wa oparesheni iliyoendeshwa katika kipindi cha miezi mitatu,kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma alisema kukamatwa kwa bunduki hizo kunatokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa Wananchi wema.

Alisema katika kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi machi,jeshi la polisi limekuwa likiendesha oparesheni za mara kwa mara na kufanikiwa kukamata bunduki hizo shortgun moja,SMG moja pamoja na magobore mawili pamoja na risasi nne zilizokuwa zikitumiwa katika matukio ya uhalifu.

Kamanda Mwakyoma alisema kutokana na oparesheni hiyo ambayo alidai itakuwa ni endelevu pia walifanikiwa kukamata siraha za jadi kama mishale,marungu,mapanga na nondo  pamoja na  watuhumiwa hamsini na sita (56) ambao walifikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Alisema katika oparesheni hiyo ambayo iliendana na misako mbalimbali katika Wilaya za Serengeti,Bunda,Musoma pamoja na Butiama walifanikiwa kukamata makosa mbalimbali na vielelezo ikiwa ni pamoja na kusambaratisha vikundi vya uhalifu vilivyokuwa vimejitokeza kwa kipindi hicho.

"Katika kipindi cha kuanzia mwezi januari mwaka huu viliibuka vikundi vitano (5) vya uhalifu katika Manispaa ya Musoma ambavyo ni Makirikiri,Jamaica mokas,Mbio za vijiti,Mdomo wqa furu pamoja na West lawama ambavyo vyote tumefanikiwa kuviosambaratisha na tutaendelea kuhakikisha hakuna kikundi chochote cha uhalifu kinakuwepo.

"Vikundi hivi kwa sasa vimetoweka baada ya kufanikiwa kusambaratishwa kwa kuwakamata viongozi wapatao 10 wa vikundi na kuwafikisha Mahakamani ambapo mpaka sasa kesi zaio zinaendelea na kiasi furani hali ya amani ipo baada ya vikundi hivyo kusambaratishwa,"alisema Mwakyoma.

Kamanda Mwakyoma alisema katika kipindi hicho cha miezi mitatu jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata watuhumiwa 62 wa madawa ya kulevya ya bangi na mirungi ikiwa ni pamoja na bangi kilo 69.6 na mirungi kilo 34.

Aliongezea kuwa katika kupambana na vitendo vya uharamia,jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 68 pamoja na vipande 26 vya pembe za ndovu ambapo watuhumiwa watano walifiokishwa mahakamani kutokana kukutwa na nyara hizo za Serekali.

No comments:

Post a Comment