Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa
wa ligi kuu soka nchini Uingereza, mashetani wekundu Manchester United
leo hii wamepiga bonge la sherehe kushangilia ubingwa wao wa 20 pamoja
na kumuaga rasmi kocha wao aliyewafundisha kwa miaka 27 na kutwaa
makombe 49 katika michuano mbalimbali.
Viongozi,
wachezaji na mashabiki wa United leo hii wamepita mitaa mbalimbali ya
jijini Manchester kushangilia ubingwa wao na kumuaga Ferguson kwa
heshima kubwa.
Kocha
Kibabu leo hii kaagwa rasmi na kubwaga manyanga ya kuwanoa United na
kazi yake kumrithisha kocha ambaye amemhusudu kwa muda mrefu, David
Moyes ambaye kwa sasa ni kocha wa Everton.

Ferguson
amesitaafu huku akiwa tayari amesharejesha ubingwa alionyang`anywa na
watani zake wa jadi Manchester City msimu uliopita na kupeleka adhaa
kubwa kwa kocha wa City, Roberto Mancini ambaye kibarua chake kinaweza
kuinga mchanga wakati wowote baada ya kufanya vibaya msimu huu.
Feguson amekaa na timu kwa miaka 27, ni ngumu kujua kama Moyes ataweza kukaa muda kama wake akiwa na United ama la.
Watu wengi walidhani Mreno Jose Mourinho angebeba mikoba ya Fergie lakini imekuwa taofauti kabisa.

Gwaride la kashangilia ubingwa lilipita katika mitaa hiyo hapo juu


Hana Furaha kabisa: Rooney alionekana kukosa furaha wakati akiwa katika basi leo








Kombe: Robin van Persie akiinua juu taji lao la 20







Source Fullshangwe
No comments:
Post a Comment