Sunday, April 28, 2013

WAKUU WA WILAYA KUCHEZA NA WABUNGE , NI KUCHANGIA KAMPENI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUSAIDIA ALBINO

……………………………………………..
Wakuu wa wilaya nchini wameandaa michezo miwili ya itakayokutanisha timu yao na timu ya Wabunge itakayofanyika mjini Dodoma na Dar es salaam mwezi wa sita mwaka huu.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakuu wa wilaya za Kibondo Venance Mwamoto na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa wamesema michezo hiyo ni   ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika kusaidia watoto mbalimbali wenye ulemavu wa ngozi Albino.

Wameongeza kwamba waamuziki wa Michezo hiyo watakuwa kama hivi Ndugu Reginald Mengi atakuwa mwamzui wa kati na wakati msaidizi wake atakuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Uratibu na Mahusiano Steven Wasira na Vibendera vitapeperushwa na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu TFF anayemaliza muda wake Leodiger Tenga pamoja naye Hafidh Ali kutoka Zanzibar

Wamesema Lengo la Michezo hiyo  ni kukusanya kiasi cha fedha kufikia shilingi milioni 300 kupitia udhamini wa makampuni mbalimbali yatakayojitokeza kudhamini timu za Wabunge na wakuu wa Wilaya pamoja na gharama zingine na fedha hizo zitakabidhiwa kwa Mh. Waziri Mkuu  kwa ajili ya kusaidia Albino.

Source:Fullshangwe

No comments:

Post a Comment