Monday, April 29, 2013

TAZAMA HALI ILIVYOKUWA HUKO ARUSHA -TANZANIA

Umati wa wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kufuatilia kesi ya Lema           Arusha, Tanzania
MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema ameachiwa kwa dhamana mpaka tarehe 29 mwezi wa tano kesi hiyo itakaposikilizwa tena katika Mahakamana hiyo.
Baada ya Mbunge huyo kuachiliwa huru, umati wa wanachama wa Chadema waliokuwa wamejazana katika Mahakama hiyo walifanya maandamano makubwa kwenda katika Ofisi za Chama hicho zilizopo maeneo ya Ngarenaro.

Mbunge huyo amekutwa na makosa matatu ambapo kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa.

Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa "Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.

Kosa la tatu ni pale alipotamka kwa wanafunzi kuwa "Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’.

No comments:

Post a Comment