Saturday, April 27, 2013

MH RUTO AOMBA ICC KUAHIRISHA KESI YAKE


Bwana William Ruto

Makamo wa rais mpya wa Kenya, William Ruto, ameiomba mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iahirishe kesi yake inayodai kuwa alishiriki katika uchochezi wa mapigano yaliyofuata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007. 

Kesi hiyo imepangwa kuanza mwezi wa May huko The Hague lakini mawakili wa Bwana Ruto wanataka iakhirishwe hadi mwezi Novemba wakisema kuwa wanahitaji muda zaidi kuandaa ushahidi wao.

Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa huenda huu ni mpango wa kutaka kesi hiyo icheleweshwe.
Katika machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 watu zaidi ya 1,000 waliuawa.

No comments:

Post a Comment