Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari aina ya Mercedec benz lenye namba ya usajili T 908 ABZ semitrailer kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kumuyange nje kidogo ya mji wa Ngara mkoani Kagera.
Watu wawili
wamefariki dunia papo hapo na wengine
wawili kujeruhiwa baada ya gari aina ya Mercedec benz lenye namba ya usajili T
908 ABZ semitrailer lililokuwa ikitokea nchini Burundi, kuacha njia leo(April 13,2013) muda wa saa 12 jioni na
kupinduka katika eneo la Kumuyange nje kidogo ya mji wa Ngara mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi
wilaya ya Ngara Abel Mtagwa amewataja
watu hao waliofarki katika ajali hiyo kuwa ni Edward Filimon alie kuwa akiendesha
pikipiki yake yenye namba za usajiri T 756 BZJ na abiria wake ambae hadi sasa
haja fahamika jina lake.
Kamanda Mtagwa
amewataja majeruhi wa ajari hiyo kuwa ni Dereva wa gari hilo Hajji Omary
Ibrahim(29) mkazi wa gongolamboto jijini Dar es salaam na tingo wake aliyejulikana
kwa jina la Kambi simba(40).
Kamanda Mtagwa
ameongeza kuwa katika ajal i hiyo nyumba moja mali ya Bi.Bibiana John (58) imegongwa
na gari hilo na kuharibika.
Aidha Kamanda
Mtagwa amesema kuwa chanzo cha ajari hiyo ni
gari hilo kufeli mfumo wa Breki jambo ambalo Dereva wake alishindwa kulimudu
kuliendesha ndipo lilipanda mtaro na kubomoa nyumba hiyo.
Aidha Majeruhi
wa Ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Murugwanza wilayani Ngara.
No comments:
Post a Comment