Friday, February 8, 2013

MAUAJI MARA

MARA

Jeshi la Polisi Mkoani Mara Linawashikili Watu wawili katika matukio mawili tofauti  ya mauaji yaliyotokea katika  wilaya za Butiama na Serengeti mkoani humo


jeshi la Polisi Mkoani humo linamshikilia   Balozi  kutoka kata ya Etaro Alex Nyarukamo mwenye umri wa miaka 61 baada ya Kukutwa nyumbani kwake kwa Pikipiki ya Marehemu Magere Mugeta yenye namba za usajili T.509 BCE.

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mara,Kamishina msaidizi  Mwandamizi Abslom Mwakyoma amesema kabla ya kuuwawa kwa Mwendesha pikipiki huyo alimgonga mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Majani katika kijiji cha Nyegina na kukimbia akidhani ameua

Katika tukio linguine Kamanda Mwakyoma amesema mtu mmoja ameuawa katika kata ya Machochwe wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa kile kinachodaiwa  ni wivu wa Mapenzi ambapo  mtuhumiwa wa Tukio hilo Mwita Wambura amejisalimisha Polisi.

Kamanda amesema Upelelezi juu ya Matukio hayo umeanza kufanyika ili kubaini na kuwabaini wahuska wa matukio  hayo na kuwachukulia hatua za kisheria  huku akitoa wito kwa Madereva wa Pikipiki watii sheria bila kushurutishwa na waepukekujichukulia sheria.

No comments:

Post a Comment