Watu saba wamefariki dunia na wengine 48
wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya Mwanza
Coach lenye namba T 736 AWJ lilikuwa
likitokea Musoma kuelekea jijini Mwanza na Basi la Best Line Lenye namba T535 AJR ambalo lilikuwa
likitokea Mwanza kuelekea Tarime
mkoani Mara
kamanda
wa polisi mkoa wa Mara kamishina Msaidizi,Mwandamizi
Absalom Mwakyoma amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana Majira ya saa kumi
na moja jioni katika barabara kuu ya Musoma - mwanza katika kijiji cha nywatari
mpakani mwa mkoa wa mara na simiyu katika wilaya ya bunda
No comments:
Post a Comment