Saturday, December 8, 2012

Uganda Mabingwa CECAFA Tusker Chalenji 2012Na Mwandishi Wetu, Uganda

TIMU ya Taifa ya Uganda, The Cranes imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Mashindano ya CECAFA Tusker Chalenji baada ya kuichapa timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars mabao 2-1.
  


Matumaini ya Kenya kutwaa kombe hilo yalizimishwa tena na Uganda baada ya kujipatia bao dakika chache kabla ya mpira kumalizika. Uganda sasa wanaendelea kuwa vinara wa kombe hilo baada ya kulitwaa mara ya 13 wakiwa wanaongoza.

Timu ya mpira wa miguu ya Zanzibar Heroes kutoka mjini Zanzibar yenyewe imefanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika mashindano ya CECAFA Tusker Chalenji baada ya kuifunga Kilimanjaro Stars mabao 6-5. Zanzibar imeifunga Kili Stars ya Tanzania bara baada ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kumalizika dakika 90 huku timu zote zikiwa sare ya 1-1. Ndipo mpambano huo ukaariwa zipigwe penati kumpata mshindi wa nafasi ya tatu.

No comments:

Post a Comment