Monday, December 31, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TELEGRAM:  “POLISI DODOMA”                                                       OFISI YA KAMANDA WA POLISI,    SIMU:2321760/2324126.                                        MKOA WA DODOMA, 
FAX    NO.    2323359.                                                                                     S.L.P   912,
e-mail:rpcdodoma@yahoo.com                                                                                                                     DODOMA 
                                                                                                                                                    

                                                  30/12/2012

DODOMA DECEMBER 30, 2012.

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA  LINAPENDA KUTOA WITO KWA WANANCHI WOTE KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA   ITAKAYOADHIMISHWA USIKU WA TAREHE 3I/12/2012 KUAMKIA TAREHE 1/12/2013 KWA AMANI NA UTULIVU, PASIPO VITENDO AMA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI NA  SHERIA ZA NCHI.
IKUMBUKWE KUWA, WANANCHI WENGI  HUTUMIA MUDA HUO KWENDA KUMSHUKURU MUNGU KATIKA NYUMBA ZA IBADA KWA MAMBO MBALIMBALI AMBAYO MWENYEZI MUNGU AMEWATENDEA KWA KIPINDI CHOTE CHA MWAKA.
PAMOJA NA HILO KUTAKUWA NA  MUENDELEZO WA SHEREHE HIZO KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA STAREHE. HATA HIVYO, UZOEFU UNAONYESHA KUWA BAADHI YA WATU HUTUMIA KIPINDI HICHO CHA SIKUKUU KUFANYA MATUKIO YA UHALIFU. 

JESHI LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA HOFU WANANCHI WOTE KUWA, LIMEJIPANGA KIKAMILIFU. KUKABILIANA NA YEYOTE YULE MWENYE NIA YA KUTENDA KITENDO CHOCHOTE CHA UVUNJIFU WA AMANI. ULINZI UTAIMARISHWA KWENYE MAENEO YOTE YA IBADA, SEHEMU ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE YOTE AMBAYO YATAKUWA NA MIKUSANYIKO MIKUBWA YA WATU.

AIDHA, TUNAPENDA KUWATAHADHARISHA KWA WALE WOTE AMBAO WATAKUWA WAKITUMIA BARABARA, KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA HASA KWA MADEREVA KUEPUKA KWENDA MWENDO KASI NA KUTUMIA VILEVI. TUTAKUWA WAKALI NA TUTAPIMA MADEREVA KILEVI.

KWA WALE WENYE KUMBI ZA STAREHE, WAZINGATIE SHERIA NA UHALALI WA MATUMIZI YA KUMBI ZAO KATIKA UINGIZAJI WA WATU KULINGANA NA UWEZO WA KUMBI HIZO, BADALA YA KUENDEKEZA TAMAA YA FEDHA KWA KUJAZA WATU KUPITA KIASI.

VILEVILE, WAZAZI WAWE MAKINI NA WATOTO WAO NA HASA DISKO TOTO AMBAZO ZIMEKATAZWA ILI KUEPUKA AJALI NA MATUKIO MENGINE YANAYOWEZA KUSABABISHA MADHARA JUU YAO. WASIRUHUSIWE KUTEMBEA PEKE YAKE BILA KUWA NA MTU MZIMA.

JESHI LA POLISI LINATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE KWAMBA, WATOKAPO KWENYE MAKAZI YAO WASIACHE NYUMBA WAZI AMA BILA MTU NA WATOE TAARIFA KWA MAJIRANI ZAO, NA PALE WANAPOWATILIA MASHAKA WATU WASIOWAFAHAMU WASIKAE KIMYA BALI WATOE TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ILI HATUA STAHIKI ZIWEZE KUCHUKULIWA HARAKA KWA WAHUSIKA.

MWISHO, WALE AMBAO HUPENDA KULIPUA FATAKI (FIRE WORKS) WAHAKIKISHE WANATUMIA ZILE ZENYE MILIO MIDOGO KWANI ZENYE MILIO MIKUBWA HULETA HOFU KWA TU HASA WAGONJWA AMBAO HUPATA MATATIZO MAKUBWA  ZAIDI.  PIA NI MARUFUKU KUCHOMA  MATAIRI BARABARANI, KURUSHA MAWE KWENYE NYUMBA NA MAGARI YA WATU.  SOTE TUTII SHERIA BILA SHURUTI ATAKAYESHINDWA KUTOKANA NA SABABU ZAKE TUTAMSHURUTISHA KWA KIWANGO KINACHOSTAHILI.

NAWATAKIENI WAKAZI WOTE WA MKOA WA DODOMA SIKU KUU NJEMA.
ASANTENI[D. A. MISIME – ACP]
KAMANDA WA POLISI [M] DODOMA

No comments:

Post a Comment