Monday, November 26, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIMsanii Maarufu na aliyekuwa anakuja kwa kasi katika muziki na pia matangazo ya biashara likiwemo la Airtel Money la kampuni ya simu ya Airtel aliyejulikana kwa jina la Sharobaro a.k.a Sharo Milionea amefariki dunia leo.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha  kutokea kwa  kifo cha  wa Sharobaro, kufuatia  ajali ya gari  katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga  ambako ndio nyumbani kwao.

Taarifa zinasema kuwa Hussein Ramadhani au Sharo Milionea alikuwa akiaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la ajali  gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza.

Katika eneo hilo inasemekana hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea,.

Blog ya Mwana wa Afrika imepokea habari hizi kwa mshtuko na masikitiko makubwa kwani nyota ya Sharo Milionea ndiyo ilikuwa inaanza kung'ara katika anga za muziki pamoja na matangazo ya biashara, akiwa kayapumulia pumzi mpya wa ubunifu na weledi katika kupeleka ujumbe kwa watazamaji ambao wakubwa na wadogo walimpenda.                                                R.I.P  Sharo

No comments:

Post a Comment