Saturday, November 3, 2012

HARAMBEE YA KUCHANGIA KANISA KUU LA PAROKIA MPYA YA UTEGI

Katika Harambee hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 35 zilipatikana huku Mifugo kama Mbuzi na Ng’ombe zikitolewa piambali na hivyo Vifaa vya Ujenzi Vilitolewa katika Harambee hiyo huku Mbunge wa Jimbo hilo Lameck Airo na Diwani wa Kata ya Roche Mh Ochele wakisema kuwa katika uchaguzi mkuu ujao hawatagombea tena katika nafasi hizo
 Mbunge wa jimbo la Rorya Mh Lameck Airo Kulia akiwa na Diwani wa kata ya Roche Mh Ochele ambapo kwa pamoja wamesema hawatagombea tena katika nafasi hizo mwaka 2015





Na Mwandishi wetu,Rorya


Mbunge wa jimbo la Rorya mkoani Mara Lameck Airo,juzi alisababisha waumini wa kanisa katoliki parokia mpya ya Utegi na mamia ya wananchi walikuwa kanisani hapo,kuangua vilio baada ya kutangaza kung’atuka katika siasa na kwamba hawezi kugombea tena ubunge.


Kwa sababu hiyo mbunge huyo,alisema pamoja na kuacha siasa na kuacha kugombea ubunge,lakini atazidi kuwa mwanachama mwaminifu wa ccm kwa kushirikiana na wenzake katika kuhakikisha kinashinda katika chaguzi mbalimbali zijazo.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Rorya Charles Ochele,ndio alianza kuwafanya waumini hao kuwa katika nyuso za uzuni na wengine kububujikwa na machozi baada ya kuitwa na mbunge huyo kwaajili ya kuchangia ujenzi wa kanisa kuu la parokia ya Utegi.


Kabla ya kutoa mchango wake wa mifuko 100 ya saruji na kiasi cha milioni sita,Ochele ambaye ni diwani wa CCM kata ya Roche, alisema wameamua kusitaafu siasa na sasa nguvu zinaelekezwa katika kuchangia nyumba za ibada.


“Nimekuja kumuunga mkono mbunge wangu kuijenga hii nyumba ya mungu,lakini leo naona wachangiaji ni wachache tofauti na kule kwenye siasa ambao wamekuwa wakitoa fedha nyingi kutafuta vyeo ndio maana mimi na mbunge wenu tumetangaza siasa basi kwani kuna watu wamefika hadi kutusema vibaya kwa tamaa tu ya vyeo hivyo tunawapisha nao waweza kusaidia maendeleo yetu”alisema na kuongeza.


“Tunaacha siasa tukiwa tumeweka msingi mzuri katika jimbo la Rorya na sasa nguvu zetu tunazihamishia katika nyumba za ibada kwani tukifanya hivyo tutazidi kuhimalisha amani katika jimbo letu baada ya wananchi kupata neon la mungu”alisema Ochele huku wananchi na waumini hao wakibubujikwa na machozi.


Hata hivyo baada ya kukabidhi mchango huo nakumpa kisemeo mbunge huyo,Airo aliwaambia mamia ya waumini na wananchi hao ndani ya kanisa hilo kuwa tayari ametangaza kutogombea ubunge mwaka 2015 ili kutoa nafasi kwa wananchi wengine wa wilaya ya Rorya kupokea kijiti hicho kauli ambayo ilionekana kupingwa na wananchi huku wengi wakionyesha nyuso za uzuni.


“Nilitangaza nataka nifanye ubunge kwa miaka mitano ili niweze kutoa mchango wangu na baada ya hapo sitagombea tena ubunge nastaafu siasa kwaajili ya kukaa na familia yangu hatua ambayo nitatoa nafasi kwa mwenzangu kuendeleza hapa nilipofikia”alisema Airo.


Alisema katika moja ya vikao vya halmashauri kuu ya ccm,alitangaza uamuzi wake huo baada pia kuchukizwa na baadhi ya wanasiasa kubaguana,kutompa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi huku wengi wakipinga hatua yake ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika jimbo zima bila kubagua kata za wapinzani.


Akizungumzia ujenzi wa kanisa hilo,alisema alikubali kuongoza harambee hiyo baada ya kuridhishwa na mchango mkubwa wa madhehebu ya dini katika kusaidia sekta mbalimbali za maendeleo katika jimbo hilo.


Alisema viongozi wa dini wana kila sababu ya kupongezwa kwa jinsi walivyosadia kurejesha amani katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vya wizi wa mifugo,uporaji,ubakaji na matumizi ya dawa za kulevya ambavyo alidai vilichangia kudhorotesha hali ya amani katika wilaya ya Rorya.


“Napenda kuwapongeza sana viongozi wa dini hasa kanisa hili jinsi lilivyosaidia sekta za maji,afya,nishati ya umeme,kilimo na ufugaji katika jimbo letu jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuharakisha maendeleoo ya wananchi wetu na wilaya yetu kwa ujumla”alisema Airo.


Awali paroko wa parokia mpya ya Utegi Padri Benedict Luzangi,limewaomba viongozi wa dini kuepuka kutumia nyumba za ibada kutoa kauli za uchochezi zinazolenga kulipiza kisasi dhidi ya dini na dini nyingine ikiwa ni njia moja wapo ya kulinda amani na utulivu uliopo nchini.


Alitoa kauli hiyo wakati akitoa mahubili kabla ya kufanyika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa kuu la parokia hiyo katika mji mdogo wa Utegi wilayani Rorya.


Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nyumba za ibada na mgongo ya dini zao kutoa kauli za uchochezi vitendo ambavyo amesema hakuna dini inayoruhusu kufanya hivyo bali watu hao wanapaswa kuhukumiwa kwa matendo yao badala ya kuhusisha dini nzima na matendo hayo mauvu ambayo kwamwe hayawezi kumpendeza Mungu.


Kuhusu vurugu na matukio ya hivi karibuni ambayo yamekuwa yakihusisha baadhi ya watu wakitumia kivuli cha dini,kiongozi huyo wa kanisa katoliki amesema kamwe matukio hayo yasihusishwe na dini nzima bali vyombo vya dola vinapaswa kuwashughulikia kama wahuni ambao wanataka kutumia dini kuvuruga amani ya nchi.


Katika harambee kiasi cha shilingi milioni 35 kilipatikana ikivikiwemo vifaa vya ujenzi,mifugo kama vile ng’ombe na mbuzi  huku mbunge huyo akichangia kiasi cha shilingi milioni tano.

MBUNGE WA JIMBO LA RORYA KATIKA ZIARA YAKE YA KUTEMBELEA MIRADI ALIYOIJENGA KWA UFADHILI WAKE

 Mh Lameck Airo Mbunge wa Jimbo la Rorya akikagua Daraja lililojengwa kwa Ufadhili wake jimboni humo
 Moja ya jengo la Walimu alilolijenga katika Mh Lameck Airo,ambapo yote mawili yaligharimu kiasi cha Milioni  26
    Mh Lameck Airo akipata Maelekzo
  Watoto wa shule ya Msingi Utegi wakipata Mlo shuleni hapo
 Ukaguzi ukiendelea katika Daraja
  Moja ya Nyumba ya Walimu iliyojengwa na Mh Airo
   Mh Lameck Airo akiweka saini katika kitabu cha Kumbukumbu
 Mh alitupia maneno kidogo
 Usikuvu ulikuwa 100 kwa 100
Kwa hisani ya www.georgemarato.blogspot.co

No comments:

Post a Comment