Friday, September 28, 2012

WACHAWI RORYA KUHUBIRIWA INJILI.


Dinna Maningo,Rorya.

MBUNGE wa Jimbo la Rorya Mkoani Mara Lameck Airo (CCM) amewahaidi wananchi wa kijiji cha Nyambogo Kata ya Kitembe kupeleka wahubiri wa dini mbalimbali kwa gharama zake  kwa ajili ya  kuhubiri injili kufuatia kwa kukithiri kwa vitendo vya kishirikina hususani kitongoji cha Dagopa kijiji cha Nyambogo vya watu kufa katika mazingira ya kutatanisha na wengine kunyofolewa viungo sehemu za siri.

Akiongea kwenye mkutano wa wananchi  wa kijiji cha Nyambogo hapo jana uliohitishwa na Diwani wa Kata ya Kitembe Thomas Patrick ( Chadema) Mbunge Airo alisema  kuwa amefikia uwamuzi huo wa kupeleka  wahubiri baada ya kupata malalamiko ya wananchi  kuwa kuna wachawi wamekuwa wakiuuwa watu kwa mazingira ya kutatanisha  huku miili ya watu wengine  wakiwa wamekufa wakikutwa  wamenyofolewa viungo mbalimbali katika sehemu za siri.


‘’ Ni aibu  kwa Rorya kusikia kuwa bado  uchawi unaendelea! Sasa hivi  watu wa Rorya tunaogopwa ukikaa na mtu akajua wewe ni Mjaruo anakukimbia anaogopa wajaruo kwamba ni wachawi watamroga sitaki Rorya ichafuke kwa uchawi nitareta wahubiri Nyambogo  na ikiwezekana makanisa mengi yanjengwe ili  watu wamwabudu mungu” alisema Airo.

Aliongeza” kwakuwa nimepata  malalamiko yenu ya kijiji chenu kukithiri  kwa uchawi  na kwamba kuna watu  wamekufa  kwa imani za kishirikina  huku wengine  kunyofolewa viungo vyao sehemu za siri nitatafuta wahubiri wa madhehebu mbalimbali  nitawagharamikia  ili waendeshe oparesheni sangara ya mahubiri wachawi wote waombewe ili waachane na ushirikina”alisema Airo.

Pia kupitia mkutano huo Mbunge huyo aliwataka wachawi wote kuachana na vitendo vya kishirikina  kwani kuendelea kufanya hivyo ni kusababisha familia zao kutengwa na jamii hususani watoto ambao ni wanafunzi ambao uogopwa na wenzao na kutengwa kutokana na uchawi wa wazazi wao.

Airo aliwataka wananchi  kupunguza hasira zao na kuwaomba  kuwapokea wachawi waliofukuzwa na wana kijiji ili Serikali ifuatilie mienendo  yao kwa ukaribu  kutokana na madai hayo ya watu kujihusisha na vitendo vya kishirikina kwani watu hao walifukuzwa na wananchi kijijini hapo ambapo walikimbilia ofisi ya DC wa Rorya Elias Goroi kuomba kuhifadhiwa.

“ Wananchi  naomba kwa sasa muwasamehe muwapokee atakaeendelea na ushirikina  wanakijiji mkamateni  msimpige  nipigieni  simu kisha tutaambatana  hadi kituo cha polisi  Utegi kama nikuwekwa ndani tuwekwe wote watafute mahali  pakuwapeleka kwa kufuata sheria za uchawi ili Dc  amuhamishe  nje ya Wilaya na ikibidi nje ya Mkoa”alisema Airo.

Mtendaji wa Kata ya kitembe Chrizan midega alisema kuwa vitendo vya kishirikina  vinavyofanywa na wachawi vimekuwa vikiwakera wananchi ambapo kupitia mkutano  wa wananchi na wazee wa mila Septemba 11 waliamuru watu hao wahame kutoka ndani ya kijiji ndani ya siku 3.

Hata hivyo kutoka na asira kali za wananchi  mnamo Septemba 14 saa saba mchana  walichoma moto miji 11 ya watuhumiwa wa uchawi   hali iliyowasababisha watuhumiwa  52 wakiwa na watoto 80 kukimbilia ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Septemba 14 kuomba hifadhi  ambapo walihifadhiwa kwa siku 2 na kisha Dc Kuamuru warejeshwe kijijini  kwao.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya Elias Goroi alisema kuwa aliamuru watu hao warejee na kuishi kijijini Nyambogo kwa madai kuwa  hakuna taarifa zozote zilizofikishwa ofisini kwake za kuwatuhumu watu wanaojihisisha na vitendo vya kishirikina  ambapo pia  aliwataka wananchi kufuata  taratibu ili anapobainika mchawi achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na mtu huyo kuhamishwa nje ya Wilaya yake.

No comments:

Post a Comment