Thursday, August 2, 2012

WAANDISHI MARA KUWAFUATA WANACHUO WA BUHARE KESHO

Na Shomari Binda
Musoma,

Kikosi cha maangamizi cha timu ya soka ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara kesho kitashuka katika uwanja wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare nje kidogo ya Manispaa ya Musoma kucheza mchezo wa kujipima nguvu ikiwa ni maandalizi ya Bonanza la michezo litakaloandaliwa na Waandishi wa Habari wa Mkoa huo katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhni.

Akizungumzia mchezo huo nahodha msaidizi wa kikosi cha wanahabari Mara Augustine Mgendi amesema maandalizi yote kuhusiana na mchezo huo yamekwisha kukamilika na kikosi kizima cha timu hiyo kipo tayari kwa ajili ya kukabiliana na wanachuo hao.
 Augustine Mgendi akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya timu ya NBC


Amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri baada ya kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo na ameahidi kikosi hicho kufanya vizuri katika mchezo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika michezo yao iliyotangalia katika siku za nyuma.

Ameongeza kuwa tayari kikosi cha maangamizi cha timu ya wana habari kimeshawekwa hadharani ambacho kitashuka dimbani hapo kesho kwa ajili ya mchezo huo ambao umekuwa ni gumzo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Musoma kutokana na tambo kutoka upande wa timu zote mbili.

Mgendi amewataja wachezaji watakaoanza katika mchezo huo kuwa ni kipa Cales Katemana,Makiwa Jumanne,Mabere Makubi,,George Maratu,Thomas Dominic,Paschal Michael,Lima Masinde,Richard Luhende,Shomari Binda,Augustine Mgendi pamoja na Fazil Janja.

Wachezaji wengine wataokuwa katika kikosi hicho ni Patrick Derick,Ahmed Nandonde,Emanuel Chibasa,Bigambo Jeje,Maxmilian Ngesi,Ahmad Kitumbo,Maxmilian Dominick,Dick Mohamed pamoja na Robert Simkoko.

                           Kikosi cha wanahabari Mara
 
Huu utakuwa mchezo wa pili katika siku za hivi karibuni kwa kikosi hicho cha wanahabari Mara ambapo katika mchezo uliotangulia waandishi hao waliwaadabisha wahesabu fedha wa benki ya NBC tawi la Musoma kwa kuwatandika mabao 3-0 mchezo uliofanyika katika viwanja vya posta mjini Musoma.

Kwa upande wake Katibu wa timu ya Waandishi wa Habari Mara Beldina Nyakeke akizungumzia kuhusiana na Bonanza amesema lengo lake ni kuleta hamasa ya michezo katika mji wa Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla na kuwaomba wadau mbalimbali wa michezo kutoa ushirikiano katika kufanikisha.

Amesema Bonanza hilo linatarajiwa kufanyika katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhamani kwa kushirikisha timu kutoka taasisi mbalimbali ambazo zitakuwa tayari katika kushiriki na litafanyika kwa siku moja.

No comments:

Post a Comment