SHERIA
YA TAKWIMU, SURA 351(THE STATTISTICS ACR, CAP.351
1.0
Utangulizi
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Wakala wa Serikali yenye mamlaka ya kisheria ya
kutoa takwimu rasmi nchini.
2.0 Mjukumu ya Ofisi
ya Taifa ya Takwimu yameainishwa katika Sheria yaTakwimu, 2002 (Na.1, 2002).
Miongoni mwa majukumu hayo ni kuendelesha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
katika Jamhuri ya Mungano wa Tanzania(To conduct population and Housing
Census in the United Republic). Kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
Aidha
, Sheria hiyo inaelekeza kuwa katika kutekeleza majukumu ya kitakwimu ambayo
yanaihusisha Tanzania na Zanzibar, NBS itashirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu
wa Serikali ya Mapinduzi ya, Zanzibar (Office oa Chief Gornment
Statatician-OCGS). Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
3.0 Kiapo cha kutunza siri(Oath of
secrecy)
Shughuli
za NBS ni za kipekee kwa kuwa zinahusu ukusanywaji wa taarifa zinazohusu maisha
ya mtu binafsi. Kwa mantiki hiyo, taarifa hizo zinahitaji usiri mkubwa. Katika
kudhihirisha jambo hilo, sheria ya Takwimu inaeleza kuwa mtu atakaye husika
katika zoezi la ukusanyji wa takwimu ikiwa ni pamoja na takwimu za Sensa ya
Watu na Makazi, atalazimika kuapishwa (kiapo cha kutunza siri) mbele ya
Kamishna wa viapo (Commissioner for Oaths) kabla ya kuanza kazi husika. Kifungu
cha 11(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
4.0
Maofisa walioidhinishwa (authorized Officersa
Katika
kutekeleza majukumu yake, Mkurungenzi Mkuu amepewa mamlaka ya kuwaidhinisha
watu wengine kwa lengo kukusanya taarifa maalum za kitakwimu kulingana na
mahitaji.
Kifungu
cha Sheria ya Takwimu, 2002.
5.0
Amri ya Rais kuhusu kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi
Sensa
ya Watu na Makazi ni shughuli ya kitaifa ambayo katika utekelezaji inahusisha
maelekezo ya Rais wa Nchi. Sheria ya Takwimu inaeleza kuwa kabla zoezi la Sensa
ya Watu na Makazi halijafanyika, Rais anatakiwa kutoa Amri (Presidential Order)
ya kufanyika kwa Sensa. Amri hiyo inatakiwa kueleza:-
a) Tarehe ya kufanyika kwa Sensa;
b) Taarifa zitakazokusanywa katika
Sensa;
c) Namna Sensa itakavyofanyika;
d) Muda na mahali Sensa itakapofanyika;
na
e) Wahusika katika kukusanya taarifa za
Sensa
Kifungu
cha 14 cha Sheria ya Takwimu, 2002
6.0 Makosa ya Jinai
na Adhabu zake
Sheria
ya Takwimu inaainisha vitendo ambavyo ni makosa ya jinai na pia Sheria hiyo
inaweka wazi adhabu zinazoweza kutolewa kwa yeyote ambaye atakuwa ametenda
makosa hayo.
Kifungu
cha 27 cha Sheria ya Takwimu, 2002 kinabainisha makundi ya aina tatu ya watu
wanaoweza kushtakiwa kutokana na viten do ambavyo ni makosa kwa mujibu wa
Sheria hiyo.
6.1 Waajiriwa wa NBS/
Wadadisi/ Wasimamizi(Authorized Officer)
a. Kutumia taarifa za kitakwimu kwa
manufaa binafsi (use of information for personal gain);
b. Kutoa taarifa za kitakwimu bila
kibali (publishing any information without authority);
c. Kutoroka/kutelekeza kazi
uliyopangiwa kuifanya (desertion);
d. Kudai taarifa
tofauti na zilizoruhusiwa kukusanywa (obtaining information not authorized to
obtain); na
e. Kuomba
malipo/ujira(asking payment or reward).
Vitendo
hivyo vyote ujumla ni makosa ya jinai na mhusika akipatikana na hatia
atastahili adhabu ya kifungo cha miezi 12 au kulipa faini ya shilingi
milioni moja au vyote viwili. Kifungu cha 27(1) a-e) cha Sheria ya Takwimu,
2002.
6.2 Kutoa taarifa
zilizopatikana isivyo halali (Mtu yeyote)
Sheria
hii inabainisha kuwa ni kosa kwa mtu yeyote kukutwa au kutoa taarifa za
kitakwimu zilizopatikana kwa kukika vifungu vya Sheria ya Takwimu. Adhabu kwa
makosa ya kundi hili ni kifungo cha miezi 18 au faini ya shilingi milioni
moja na laki tano au vyote viwili. Kifungu cha 27(2) cha Sheria ya Takwimu,
2002
6.3 Kutotoa
ushirikiano katika zoezi la kitakwimu (Respondent/ Mtu yeyote)
Sheria
hii pia inaainisha makosa yanayowezakufanywa na mtu yeyote au Respondent wakati
wa zoezi la kitakwimu (wakati wa kukusanya takwimu). Makosa hayo ni:
a. Kumzuia
Authorized Officer (Msimamizi/Mdadisi/Karani wa Sensa kutekeleza majukumu yake
b. Kukataa /kuacha
kwa makusudi:
i. Kujaza fomu au
nyaraka yoyote iliyokabidhiwa kwake kwa lengo maalum;
ii. Kujibu maswali aliyoulizwa;
c. Kutoa taarifa za
uongo
d. Kuharibu au
nyaraka yoyote
e. Kujifanya
Authorized Officer kwa lengo la kujipatia taarifa ambazo hastahili kuzipata;
f. Kukataa kutoa
nyaraka zozote zinazohitajika katika shughli za kitakwimu;
g. Kukiuka kifungu
chochote cha Sheria hii.
Sheria
inaeleza kuwa adhabu kwa kosa lolote kati ya hayo ni kifungo cha miezi 6 au
faini ya shilingi laki sita. Kifungu cha 27(3) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
7.0 Hitimisho
Sheria
ya Takwimu, 2002 imeainisha majukumu ya NBS na kutamka wazi aina za makosa na
adhabu zake.
Kwa
mantiki hiyo ni kjukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake na kutoa ushirikiano
unaostahili katika zoezi la Sensa ya Watu ma Makazi ya Mwaka 2012.
Kwa
kufanya hivyo, kila mdau atakuwa ameisaidia Serikali kupata taarifa sahihi kwa
ajili ya mipango ya maendeleo ya nchi.
SENSA
KWA MAENDELEO: JIANDAE KUHESABIWA
No comments:
Post a Comment