KOCHA Arsene Wenger amesema kwamba Arsenal haikuwa na nguvu ya kumzuia Robin van Persie kusaini Manchester United.
United iliipata saini ya mchezaji huyo jana usiku, baada ya Arsenal
kukubali kumuuza Van Persie wapinzani wao wa taji la Ligi Kuu kwa pauni
Milioni 24.
Baada ya wiki kadhaa za majadiliano na Arsenal na mshambuliaji huyo
wa Uholanzi, United imewapiku Manchester City na Juventus mbi za
kuwania saini ya Van Persie mwenye umri wa miaka 29 na leo atafanyiwa
vipimo vya afya Old Trafford.
‘Inauma kumpoteza mchezaji wa ubora wake. Tulikuwa tumebakiza mwaka
mmoja tu katika mkataba wake, hivyo hatukuwa na chaguo,’alisema Wenger.
No comments:
Post a Comment