Musoma
Chama
cha walimu (CWT) Mkoa wa Mara kimewasihii walimu kutohadaika na kauli
ya Serikali ya kuwataka kutogoma kwani haki zao bila kuchua hatua hiyo
kamwe hazitatimizwa kwa wakati.
CWT imesema upatikanaji wa maslahi bora ya
kazi yatapatikana kwa kushirikiana katika mgomo utakaoanza kesho ili
Serikali ione umuhimu wa madai yao ambayo wamekuwa wakiyadai kwa muda
mrefu sasa bila kupatiwa ufumbuzi.
Katibu wa CWT Mkoa wa Mara Fatuma Bakari
amesema walimu wasiwe waoga kutetea haki zao kwani mgomo huo huko
kisheria na kinachofanywa na Serikali ni vitisho kwao ambavyo amesema
havina msingi.
Bakari amewakumbusha walimu kuwa madai yao
ya maslahi bora ni ya muda mrefu huku akihituhumu Serikali kuendelea
kuyapuuzia na kuwafanya kuishi maisha duni na kifukara licha ya kufanya
kazi kubwa nayakujituma.
Uchunguzi uliofanywa na na mwandishi wa
blogu hii Mjini Musoma umeonyesha kuwa mgomo huo hupo kesho na walimu
wengi wamenukuliwa wakisema wako tayari kugoma ili kuishinikiza Serikali
kutatua kero zao wanazozidai.
Walimu hao wamesema kamwe hawawezi
kuwasaliti viongozi wao wa Kitaifa waliowachagua na kuwaachia vita hiyo
ya madai ya msingi wapigane wenyewe kama vile wanapigania maslahi yao
binafsi.
No comments:
Post a Comment