MEMBE AMLILIA KANUMBA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amemlilia Muigizaji Steven Kanumba kama Muigizaji maarufu aliyeitangaza Tanzania katika medani za kimataifa ambaye uhai wake umekatishwa ghafla.
Akizungumza katika Tamasha la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, Mhe. Waziri Membe, huku akishangiliwa na Umati wa watu alisema tasnia ya sanaa imepata msiba mkubwa kwa kupotelewa na Mwigizaji Steven Kanumba kufuatia kifo cha ghafla kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 8 Aprili,2012.
"Nimestushwa sana na msiba huo mkubwa. Kanumba alikuwa Balozi wetu mkubwa nje, umaarufu wake ulifika hata ambako nchi yetu haina Ubalozi, na kupitia uigizaje wake, ameweza kuwa mgeni wa familia nyingi kwenye sebule zao kupitia luningani. Naomba tusimame dakika moja tumuombee na kumtakia heri." alisema Waziri Membe.
Aidha, Mhe. Membe amekemea vitendo vya kifisadi na kuporomoka kwa maadili ya uongozi kama vitu visivyohitaji kuvumiliwa katika jamii ya Watanzania na kuongeza kwamba, mfumuko wa bei na kuyumba kwa uchumi wa dunia vimesababisha hali ya kukata tamaa kwa baadhi ya watu.
Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, Mhe. waziri amesema Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa zawadi ya Pasaka kwa kutangaza jopo la Watu mahili kuratibu zoezi kupata katiba mpya akiwemo Jaji Joseph Warioba na Jaji Augustino Ramadhan.
Alisema kila mtanzania mwenye akili timamu ni vema akatoa maoni yake juu aina katiba anayotaka na kwamba wawapuuze wanasiasa wowote watakaotaka kutumia fursa hii ya Wengine watatumia muda huo kuleta uchochezi, tuwapuuze.
" Tanzania tunayoitaka ni Tanzania inayomwogopa Mungu, Tanzania inayodumisha upendo, Tanzania inayovumilia imani na dini mbalimbali, Tanzania isiyobaguana na Tanzania yenye neema tele zitokanazo na rasilimali zake, Tanzania ambayo kila mtu ana fursa ya kuchangia maendeleo na kuneemeka na fursa zitokanazo na mchango wake." Alisema Mhe. Membe.
Aidha, katika Tamasha hilo Mhe. Membe pamoja na marafiki zake walichangia jumla ya shilingi 25 milioni kati ya hizo milioni 10 toka kwa Membe na marafiki aliongozana nao, milioni 10 toka kwa Mhe Rais Kikwete na Milioni 5 kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.
Tamasha hili lilihusisha wanamziki maarufu wa nyimbo za injili kutoka nchi mbalimbali akiwemo Solomon Mukubwa, Anastazia na Upendo Kilahira toka Kenya, Rebecca Malope toka Afrika ya Kusini, Rose Mhando na Christina Shusho toka Tanzania pamoja na mwanamziki kutoka Zambia

No comments:
Post a Comment