HABARI KUTOKA TARIME MKOANI MARA
BARAZA la mamlaka ya mji mdogo wa Tarime mkoani Mara,limeitaka idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Tarime kuacha mara moja tabia ya kuwauzia watu binafsi maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule na huduma nyingine za jamii.
Kwa mujibu wa wajumbe wa baraza hilo,idara hiyo ya ardhi imekuwa ikiuza ovyo maeneo hayo kwa watu binafsi wakiwemo viongozi wa kiasiasa jambo ambalo limechangia kuzuoa migogoro na kukwamisha ujenzi wa shule katika maeneo hayo.
Wakichangia katika kikao hicho cha dharura ambacho pia kimehudhuriwa na mbunge wa jimbo hilo Mh Nyambari Nyangwine,chini ya uenyekiti wa Christopher Mantago kwaajili ya kuzungungumzia kero mbalimbali katika mamlaka hiyo,wamesema endapo hatua hazitachukuliwa kwa kuzuia idara ya ardhi kuuza maeneo hayo kuna hatari ya kuja kusababisha machafuko ambayo yanaza kuzuilika.
Hata hivyo akizungumza katika kikao hicho mbunge huyo wa Tarime,ameahidi kulishughulikia suala hilo kwa kuanzia katika maeneo ya saba saba ili kupatikana eneo la kujenga shule ya Sekondari ambayo itawaondolea kero watoto wanaishi kata hiyo lakini wanalazimika kwenda kusoma kata jirani.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
WATENDAJI wa vijiji na kata katika wilaya ya Tarime mkoani Mara,wametakiwa kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi kila wakati na kuelezea utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili kujenga imani na kuwafanya wananchi kuchangia miradi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilayani Tarime Bw Bogomba Rashid katika ziara yake ya siku 18 ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho wilayani Tarime na kuhamasisha wanachama wake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.
Amesema kuwa ni wajibu wa viongozi hao kutoa taarifa hizo za mapato kwa wananchi na utekelezaji wa miradi hiyo katika maeneo yao jambo ambalo pia litawaondolea wasiwasi wananchi dhidi ya utendaji kazi wa viongongozi wao.
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa ccm wilaya ya Tarime,amewataka viongozi hao wa vijiji na kata kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ambayo itaweza kuwangozea kipato wanmanchi wao pia kutatua kero zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment