Friday, February 24, 2012

HABARI KUTOKA MARA

MUSOMA

WAFANYABIASHARA WA DAGAA KATIKA SOKO LA MWIGOBERO, MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA, WAMELALAMIKIA KUTOZWA USHURU WA SHILINGI 1000, BADALA YA SHILINGI 300 KWA KILA MZIGO BILA KUPEWA STAKABADHI NA MZABUNI AMBAYE AMEPEWA KAZI YA KUKUSANYA USHURU WA MANISPAA HIYO.

WAKIZUNGUMZA SOKONI HAPO  BAADHI YA WAFANYABIASHARA WAMESEMA KUWA MZABUNI HUYO AMEKUWA AKIPANDISHA USHURU KILA KUKICHA HUKU AKITOA RISTI YA SHILINGI MIA TATU HATUA AMBAYO IMEKUWA IKISABABISHA MGOGORO MKUBWA.

MIONGONI MWA WAFANYABIASHARA HAO BW JOSEPH NYANGASI NA BW SHABAN MATUMBO,WAMESEMA KITENDO CHA KUWATOZA USHURU HUO MKUBWA BILA STAKABADHI KUTOKA SHILINGI MIA TATU ZA AWALI HUKU AKISHINDWA KUBORESHA HUDUMA KATIKA ENEO HILO NI UONEVU NA WIZI MKUBWA UNAOTAKIWA KUCHUKULIWA HATUA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA.

KWA UPANDE MZABUNI HUYO WA UKUSANYAJI WA USHURU DAGAA NA SAMAKI PAMOJA NA MAZAO MENGINE YANAYOUZWA KATIKA SOKO HILO BI ALICE JUMANNE,AKIZUNGUMZIA MADAI HAYO AMESEMA KINACHOFANYIKA NI KUSIMAMIA TARATIBU NA SHERIA KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO.

NAYE  MKURUGENZI WA MANISPAA YA MUSOMA, BW. NATHAN MSHANA AMESEMA USHURU HUO NI HALALI, NA KAMA KUNA MFANYABIASHARA YEYOTE ANAYETILIA SHAKA KIWANGO HICHO AWASILISHE MALALAMIKO OFISINI KWAKE.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

SERENGETI

MKOA WA MARA UMETANGAZA MIKAKATI MITANO YA KUPAMBANA NA KASI KUBWA YA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA UKIMWI,IKIWA NI PAMOJA NA KUZUNGUMZA KWA UWAZI,KULAANI NA KUWAFANANISHA KAMA WAUAJI WATU WOTE WANAONEZA VIRUSI HIVYO KWA WENZAO KWA MASUDI.

KAULI HIYO IMETANGAZWA NA MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN GABIEL TUPA,KATIKA KIJIJI CHA NYAGASENSE KATA YA KENYAMONTA WILAYANI SERENGETI,BAADA YA KUZINDUA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA KWA WAGONJWA WALIO ATHIRIKA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.

MKUU HUYO WA MKOA AKIZUNGUMZA BAADA YA KUZINDUA JENGO HILO NDANI YA KITUO CHA AFYA CHA IRAMBA,AMBALO LIMEJENGWA  KWA USHIRIKIANO WA SHIRIKI LA KUDHIBITI MAGONJWA CDC,AIDS RELIEF  KUPITIA UFADHGILI WA MPANGO WA DHARURA WA RAIS WA MAREKANI WA KUDHIBITI UKIMWI.

AMESEMA MKOA WAKE HIVI SASA UNAONGOZA KITAIFA KWA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI KWA KUWA NA CHA ASLIMIA 7.7, UNAWEZA KUPUNGUZA KASI HIYO ENDAPO KILA MTU ATAJITHAMINI,KUJIPENDA NA KUWAKINGA WENGINE.


KWA UPANDE WAKE MENEJA MWANDAMIZI AIDS RELIEF  DK EKANDUMI KIMOI,AMESEMA SUALA LA TIBA MBADALA MAARUFUKAMA KIKOMBE CHA BABU,LIMEKUWA NA CHANGAMOTO KUBWA AMBAYO IMESABISHA IDADI KUBWA YA WAGONJWA KUSITISHA MATUMIZI YA DAWA HIVYO KUSABABISHA WENGI WAO KUFARIKI DUNIA HUKU WANGINE WAKIWA KATIKA HALI MBAYA

NAYE MTAALAM WA AFYA YA JAMII WA UKIMWI NA KIFUA KIKUU KUTOKA SHIRIKA LA KIMAREKANI LA KUDHIBITI MARADHI NA KINGA DK GODWIN MUNUO,AMESEMA KUJENGWA KWA KITUO HICHO NI UKOMBOZI MKUBWA KWA WANANCHI WA ENEO HILO WANAOFIKIA ZAIDI ELFU 13 HUKU AKITOA WITO KWA WATU WALIO ATHIRIKA KUTUMIA HUDUMA NA TIBA KWA WAKATI NA KUWAHIMIZA NDUGU NA MARAFIKI KUTAMBUA AFYA ZAO MAPEMA.

MIONGONI MWA MIKAKATI AMBAYO IMETAJWA NA MKOA WA MARA KATIKA KUPAMBA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KUPAMBANA NA MILA ZINAZOCHANGIA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI,ZIKIWEMO ZA UKEKETAJI WANAWAKE,KURITHI WAJANE PAMOJA NA KUHIMIZA TOHARA SALAMA KWA WANAUME NA KUHIMALISHA HUDUMA ZA KUZUIA MAAMBUKIZI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BUNDA

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA MKOANI MARA IMEKANUSHA MADAI KUWA ILITEKELEZA MIRADI CHINI YA KIWANGO NA KUSEMA INAFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MIONGOZO ILIYOPO NA KUWATAKA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KURIPO KWENYE VYOMBO VYA HABARI.

KAULI HIYO IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI HIYO CYPRIAN OYEIR  KUFUATIA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA ASASI MOJA BINAFSI INAYOSHUGHULIKIA MAENDELEO KUTOAS TAARIFA KWENYE BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KWAMBA HALMASHAURI HIYO  INATEKELEZA MIRADI KATIKA JIMBO LA MWIBARA CHINI YA KIWANGO CHA UBORA.

MIRADI INAYODAIWA KUTEKELEZWA CHINGI YA KIWANGO CHA UBORA NI BARABARA ZA NERUMA HADI CHAMAKAPO YENYE UREFU WA KM 4 NA CHAMAKAPO HADI KARUKEKERE(KM 5) ZOTE ZA JIMBONI HUMO HUKU WALIOLIMA BARABARA YA NAKATUBA NANSULULI YENYE UREFU WA KM 6 WAKIELEZEWA KUIDAI HALMASHAURI HIYO IJARA YAO.

AKIELEZEA MIRADI HIYO OYEIR AMESEMA ILITEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) KWA GHARAMA YA YA SHILINGI MILIONI 31 KILA MMOJA ZILIZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MIRADI HIYO IKIWAMO YA KUNG’OA VISIKI;KUSAMBAZA UDONGO;KUSAWAZISHA TUTA LA BARABARA;KUPIMA ENEO LA KUPITISHA BARABARA;KULIMA NYASI;KUUMBA TUTA LA BARABARA NA KUWEKA MITARO YA PEMBEZONI MWA BARABARA.

MBALI NA KUIELEZEA MIRADI HIYO KUWA ILITEKELEZWA CHINI YA KIWANGO CHA UBORA ASASI HIYO PIA YENYE MAKAO YAKE MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM ILIDAI KUWEPO KWA BAADHI YA WATU WANAOIDAI HALMASHAURI HIYO UJIRA WAO KAMA MALIPO YA KUSHIRIKI KATIKA KAZI HIYO JAMBO AMBALO MKURUGENZI MTENDAJI HUYO AMELIKANA NA  AKASEMA WOTE WALILIPWA HUKU AKIONESHA NYARAKA ZA MALIPO KWA WAANDISHI.

HATA HIVYO MKURUGENZI HUYO AMESEMA PENGINE ASASI HIYO HAIKUTOFAUTISHA KAZI ILIYOFANYWA KWA MIKONO NA ILE INAYOFANYWA KWA MITAMBO NA  NDIYO SABABU YA  KUSEMA MIRADI HIYO IMETEKELEZWA CHINI YA KIWANGO CHA UBORA JAMBO AMBALO HATA HIVYO AMESEMA LINGEEPUKWA TU KAMA WANGETAFUTA UKWELI WA MAMBO HAYO KUTOKA KWA WATAALAM WA HALMASHAURI NA KUWASHAURI KUFANYA HIVYO ILI KUEPUSHA MIGONGANO KATIKA MAENDELEO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
RORYA

HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA MKOANI MARA YADAIWA KUTUMIA VIBAYA PESA ZA RUZUKU YA SERIKALI  ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 17 KWA MIEZI MITATU YA JULAI HADI SEPTEMBA 2011 ZILIZOTOLEWA KWA AJILI YA VITENGO AMBAPO IDARA SABA ZIMEDAIWA KUTUMIKA TOFAUTI.

TAARIFA KUTOKA UKAGUZI WA NDANI KWA ROBO YA KWANZA MWAKA 2011 HADI 2012 JULAI –SEPTEMBA ZINASEMA KUWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA NDANI YA HALMASHAURI YA RORYA ZIMEKIUKA KANUNI NAMBA 49 PAMOJA NA KUKWAMISHA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZILIZOPITISHWA NA VITENGO HUSIKA.

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YAMEPELEKEA KUKWAMISHA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA VITENGO KUTOKANA NA FEDHA HIZO KUTUMIWA KWENYE  SHUGHULI NYINGINE NA ZINGINE KUTOJULIKANA ZIMEFANYA KAZI GANI NA HIVYO KUSABABISHA VITENGO KUKWAMA NA KWAMBA ZIMEPUNGUZA MORALI YA KAZI.

WAKATI HUO HUO,  KAMPUNI YA NYAKILANG'ANYI IMEKIUKA MKATABA AMBAO ILIINGIA NA HALIMASHAURI YA WILAYA YA RORYA  KWA AJILI YA UJENZI WA HOSTEL YA NYANDUGA AMBAPO HALMASHAURI HIYO ILITOA ZAIDI YA SH.MILIONI 2OO KWA AJILI YA UJENZI WA HOSTELI.

HABARI ZAIDI ZINAELEZA KUWA MKANDARASI ALITAKIWA KUKABIDHI JENGO HILO MAY 30 MWAKA 2011 LAKINI MPAKA UKAGUZI UNAMALIZIKA MKANDARASI BADO HAJAKABIDHI JENGO HILO ILI HALI ZILIKUWA SIKU ZAIDI 100 ZIMEPITA NA WANAFUNZI BADO WANAKOSA HUDUMA.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

TARIME

WILAYA YA TARIME MKOANI MARA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI HALI INAYOSABABISHA BAADHI YA SHULE KUENDELEA KUWA NA UPUNGUFU WA WALIMU NAHIVYO KUSHUSHA KIWANGO CHA TAALUMA KWA WANAFUNZI.

KAIMU OFISA ELIMU GIDION MUHOCHI AMESEMA WILAYA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WALIMU 229 HALI INAYOSABABISHA BAADHI YA WALIMU KUWA NA VIPINDI VINGI MADARASANI AMBAPO WILAYA HIYO INAJUMLA YA SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI 126.

MUHOCHI AMESEMA KUWA  WILAYA ILIKUWA NA UPUNGUFU WA WALIMU  341 NA KUWA KWA MWAKA HUU WILAYA YA TARIME IMEPEWA WALIMU 117 NA KATI YA HAO WALIORIPOTO NI 112 AMBAPO WALIMU 5 BADO KATIKA SHULE WALIZOPANGIWA.

AIDHA MUHOCHI AMESEMA KUWA WALIMU WOTE WALIORIPOTI TAYARI WAMESHAPATIWA FEDHA  ZA KUJIKIMU WAKATI WA KURIPOTI KATIKA VITUO VYAO VYA KAZI NA KWAMBA KWA KILA MWALIMU AMEPATIWA  SH.LAKI 2 NA ELFU 10,000.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment