Friday, February 24, 2012

HABARI KUTOKA KANDA YA ZIWA

MUSOMA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA,IMEOMBWA KUZIONDOA GEREJI ZOTE AMBAZO ZIMEJENGWA PEMBENI MWA ZIWA VICTORIA KUTOKANA NA KUTIRIRISHA OVYO MAJI YA MABAKI YA MAFUTA NDANI YA ZIWA HILO JAMBO AMBALO LIMEDAIWA LIMEKUWA LIKISABABISHA UCHAFUZI MKUBWA WA MAZINGIRA.

WANANCHI HAO WAMESEMA KUWA BAADHI YA WATU WAMEANZISHA GEREJI BUBU KARIBU YA MAENEO YOTE YA MWALO WA MWIGOBERO HUKU WAKITUMIA GEREJI HIZO KUOSHEA MAGARI HATUA AMBAYO IMEKUWA IKICHANGIA KUINGIZA MAJI YA MABAKI YA MAFUTA NDANI YA ZIWA NA HIVYO KUSABABISHA UCHAFUZI MKUBWA WA MAZINGIRA.

HATA HIVYO WANANCHI HAO WAMESEMA MANISPAA YA MUSOMA INAPASWA KULAUMIWA KWA UCHAFUNZI HUO MKUBWA WA MAZINGIRA KUTOKANA NA KUFUMBIA MACHO SUALA HILO HUKU WAKITAMBUA WAZI KUWA MABAKI HAYO YA MAFUTA KUINGIZWA KATIKA MAJI YA ZIWA HILO YANAWEZA KUWA NA ATHARI KUBWA KWA BINADAM WANAOTUMIA MAJI HAYO PIA KUHARIBU MAZALIA YA SAMAKI.

KWA UPANDE  WAKE MWENYEKITI WA KIKUNDI CHA KUTUNZA HIFADHI YA MIAMBAO YA MAJI KATIKA MANISPAA YA MUSOMA BW OBED KASWAMILA,AMESEMA UCHAFUNZI WA MAJI YA ZIWA UMEANZA KUSHAMILI KUTOKANA NA UZEMBE MKUBWA WA MAAFISA WA MAZINGIRA KATIKA MANISPAA YA MUSOMA NA MAENEO MENGINE MKOANI MARA KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA SHERIA ZILIZOWEKWA .
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MWANZA.

MELI NDOGO YA MIZIGO YA PASIFIC, IMEZAMA KATIKA ZIWA VICTORIA, AMBAPO MTU MMOJA AMERIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, HUKU WENGINE 15 WAKIOKOLEWA NA WAVUVI NDANI YA ZIWA HILO.

MELI HIYO INAYODAIWA KUMILIKIWA NA MTOTO WA MMILIKI WA KAMPUNI YA MELI ZA NYEHUNGE JIJINI MWANZA, IMEZAMA JANA MAJIRA YA SAA 3 ASUBUHI, IKIWA INATOKA KATIKA KISIWA CHA GHANA WILAYANI UKEREWE KWENDA JIJINI MWANZA, NA IMEZAMA ENEO LA BWIRO WILAYANI UKEREWE.

TAARIFA ZINAELEZA KWAMBA, MELI HIYO ILIKUWA IMESHEHENI MIZIGO YA DAGAA, PAMOJA NA MAKRETI YA SODA NA BIA  AMBAPO INAELEZWA KUWA  CHANZO CHA KUZAMA NI DHORUBA KALI, AMBAPO MELI HIYO ILISHINDWA KUMUDU MAWIMBI HAYO MAKUBWA.

KWA MUJIBU WA TAARIFA HIZO, AMBAZO PIA ZIMETHIBITISHWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA PAMOJA NA MAMLAKA YA UDHIBITI WA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI NCHINI (SUMATRA), KANDA YA ZIWA, ZIMEELEZA KWAMBA, MELI HIYO YA PASIFIC ILIZIDIWA MAWIMBI MAKALI NDANI YA ZIWA HILO, HIVYO KUZAMA MAJI KABISA.

HILI NI TUKIO LA PILI AMBAPO JUMAPILI WIKI ILIYOPITA, BOTI MOJA YA ABIRIA ILIZAMA KATIKA ZIWA VICTORIA, WAKATI IKITOKA MAISOME KWENDA KAHUNDA WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA, AMBAPO WATU 35 WALIHOFIWA KUFA MAJI, INGAWA BAADAYE JESHI LA POLISI LILIDAI HAKUNA ALIYEFARIKI DUNIA BAADA YA ABIRIA HAO KUOKOLEWA.

MBALI NA HAYO, HIVI KARIBUNI WATU KADHAA WALINUSURIKA KUFA MAJI BAADA YA BOTI MBILI WALIZOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGANA USO KWA USO NDANI YA ZIWA VICTORIA KATIKA ENEO LA MUSOMA VIJIJINI MKOANI MARA.

AKITHIBITISHA KUZAMA KWA MELI HIYO YA PASIFIC HAPO JANA  OFISA MKAGUZI WA SUMATRA KANDA YA ZIWA, BW. ALFRED WARIANA AMESEMA, NI KWELI MELI HIYO IMEZAMA NDANI YA ZIWA HILO IKIWA NA SHEHENA KUBWA YA MIZIGO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment