MUSOMA
KUTOKANA na kuadimika kwa mafuta ya Petroli katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara,kumefanya bei ya nishati hiyo kupanda kupanda kutoka shilingi 2,060 kwa lita hadi shilingi 8,000 na shilingi 12,000 kwa lita moja.
Mafuta hayo ambayo sasa yanauzwa katika vichochoro vya Manispaa ya Musoma na watu binafsi wasio na leseni ya kufanya biashara hiyo baada ya kuyarangua kutoka katika vituo vya mafuta kuanzia juzi na jana usiku.
Asubuhi ya leo Victoria fm imeshuhudia mamia ya wananchi wakiwemo madereva wa magari na pikipiki kunzia saa kumi na moja alfajiri wakiwa katika foleni ya kununua mafuta hayo kwa gharama kubwa katika vichochoro hivyo.
Mbali na uhaba huo wa mafuta ambao umesababisha kero kubwa kwa abiria kutokana na magari na pikipiki kuegeshwa kwa kukosa nishati hiyo pia wavuvi wanaovua samaki kwa kutumia ingini za boti katika ziwa victiria upande wa mkoa wa Mara wamesimamisha shughuli zao za uvuvi baada ya kukosa nishati hiyo.
Hata hivyo wananchi hao wameiomba serikali kupitia EWURA kutangaza bei ya kudumu ambayo itatumika wakati wote badala ya kupandisha na kushushu jambo ambalo limesababisha kero hiyo kwa vile hivi sasa baadhi ya wamiliki wa vituo wanadaiwa kuficha nishati hiyo baada ya EWURA kutangaza kushuka kwa bei.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
RORYA
ENEO la urefu wa kilometa moja na upana meta 50 katika kitongoji cha Nyanchabo, kijijiniIkoma wilayani Rorya, limetitia kwa kina cha futi 25.
Ajali hiyo imesababisha hasara kubwa kwa wakulima zaidi ya 20 na wafugaji watano ambao wamepoteza mali zao wakiwamo ng’ombe, mbuzi, mazao ya chakula na miti ya mbao zaidi ya hekta 30 kuharibiwa.
Akizungumza katika eneo la ajali jana, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa, aliwaagizawaathirika hao kuondoka kwa kuwa eneo hilo limeonesha kuwa linaendelea kutitia.
Aliwataka maofisa, akiwamo Mwenyekiti wa Kijiji na Ofisa Mtendaji wa Kijiji kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Cosmas Ngangaji, kuhakikisha kuwa WATU wanaoishi kando ya bonde hilo wanahama mara moja.
AMEAgiza wananchi hao watafutiwe maeneo mengine ya kuishi katika kitongoji hicho kwa kuwa madhara mengine zaidi huenda yakatokea.
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN Tupa aMEahidi kurudi maeneo hayo na mengine katika wilaya hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao akifuatana na viongozi wa halmashauri.
No comments:
Post a Comment