Tuesday, August 23, 2011

CHADEMA WAANZA KAZI IGUNGA KWA HELKOPTA

VUGUVUGU la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora linazidi kupanda
huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikitangaza safu ya viongozi wa kitaifa watakaozindua kampeni za chama hicho Septemba 9, mwaka huu.

Mbali na kuanika majina ya viongozi wake watakaozindua kampeni, chama hicho kina mkakati wa kutumia helikopta ili kufikia maeneo yote ya Jimbo la Igunga.


"Kama kawaida yetu tayari  helikpta imeandaliwa kwa mashambulizi ya kampeni jimbo la Igunga, lakini hatutaanza nayo, tutaanza na vyombo vya ardhini kwanza tukiona kuna ulazima, ndipo tutakaponyanyuka juu kwa juu na kumwaga sumu 'chini'."


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, wakati akizungumza na gazeti la Majira kwa njia ya simu akiwa Igunga. Alisema viongozi wa kitaifa watakaohudhuria uzinduzi wa kampeni za chama hicho ni Katibu Mkuu, Dkt. Willbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Bw.Zitto Kabwe. Chanzo Gazeti Majira

No comments:

Post a Comment