Thursday, February 17, 2011

WANANCHI WALALAMIKIA MFUMUKO WA BEI NCHINI



MUSOMA

WANANCHI wa mji wa Musoma mkoani Mara wamelalamikia mfumuko wa bei unaendelea hapa nchini huku wakisema kuwa huko ni usaliti wa viongozi katika katika kuwapatia maisha bora waliyowaahidi miaka mitano iliyopita.

Wakiongea na mwandishi wa gazeti hili mjini hapa baadhi ya wananchi hao kutoka sehemu mbalimbali katika manispaa ya Musoma walisema kuwa miaka mitano iliyopita maisha yamekuwa magumu lakini badala ya viongozi kupambana na hali hiyo lakini bado ndio maisha ndiyo yanaendelea kupanda.

 “Miaka mitano iliyopita maisha yamekuwa juu sana na viongozi wakawa wanaahidi kuboresha maisha lakini hakuna kinachofanyika mpaka sasa” alisema James Marwa mkazi wa Kigera

Katika mfumuko huo wa bei ambao bidhaa zimeonekana kupanda kila kukicha,kilo moja ya Mchele  kwasasa ni shilingi elfu moja mia moja kutoka shilingi mia nane katika wiki takribani tatu zilizopita huku  kilo moja ya Sukari imepnda kutoka shilingi Elfu moja mia sita mpaka shilingi Elfu mbili.

Mbali na kupanda kwa vitu hivyo lakini bado wananchi walilalamikia kupanda kwa mafuta ya taa ambayo yanaonekana kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wasiokuwa na nishati ya umeme hapa nchini,Mafuta hayo inasemekana yamepanda kutoka shilingi mia Tano kwa chupa ya Fanta mpaka kiasi cha shilingi mia nane.

Aidha hivi karibuni kumekuwepo kwa taartifa ya kupanda kwa bei ya usafiri kwa mabasi ya mikoani na ndani ya mji kitu ambacho kinaonekana kuwa pigo lingine kwa wananchi katika kipindi cha wiki chache tangu kupanda kwa mahitaji muhimu.

Pamoja na kupanda kwa baadhi ya mahitaji muhimu katika maisha ya kila siku wananchi hao walisema kuwa kuna kila sababu kwa serikali kuingilia kati mfumuko huo wa bei kwani unawaumiza wananchi wa hali ya chini.

 “Kama serikali haitainfgilia kati suala zima la mfumo hapa nchini tutakufa jamani maana hata kupata shilingi elfu moja leo ni tabu na haitoshi kununua kitu sasa maisha gani haya” alisema Marwa Weitara mkazi wa Nyakato.

Wananchi hao wa Manispaa ya Musoma waliongeza kuwa si mahitaji muhimu katika maisha pekee bali hata gharama ya shule mbalimbali za binafsi nazo ni tatizo kwa kupandisha bei bila kuangalia kipato cha mtanzania wa sasa.

Kufuataia hali hiyo wananchi hao walisema kuwa ni vyema Rais Kikwete akawatazama wananchi wenye kipato cha chini kwani wao ndio wengi kuliko walionacho ili kupunguza nafasi kati ya aliyenacho na asiyekuwa nacho.

mwisho

No comments:

Post a Comment