Tuesday, February 8, 2011

ASASI ZATAKIWA KUPAMBANA NA UKIMWI

SERIKALI mkoani Mara amezita asasi zote za zinazopambana na maambukizi ya Ukimwi Mara kushirikiana na viongozi katika ngazi zote za mkoa wa Mara kukemea kwa nguvu zote vitendo vya ukatili,udhalilishaji wa jinsi,mila na desturi ambazo zinachangia kasi ya maambuzi ya VVU mkoani hapa.
Kauli ya serikali ya mkoa wa Mara imekuja baada ya mkoa wa Mara umetajwa kuwa wanne kitaifa kwa kuwa na kasi kubwaya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka asilimia nne miaka mitatu iliyopita hadi kufikia asilimia 7.7 ikiwa ni juu ya maambukizi ya asilimia 57 ya kitaifa.
Mkuu wa mkoa wa Mara kanali mstaafu Enos Mfuru,alisema hayo jana mjini Musoma wakati akifungua warsha ya siku moja ya kupanga mipango ya mkoa na halmashauri za mkoa huo kwaajili ya kupunguza maambukizi ya VVU mkoani Mara.
Alisema utafiti ambao ulifanywa na ofisi ya taifa ya takwimu mwaka 2007/8 unaonesha kuwa maambukizi ya kitafa ni wastani wa asilimia 5.7,wanawake ikiwa ni asilimia 6.9 na wanaume ni asilimia 4.5.
Alisema kuwa utafiti huo unaonesha kuwa katika maeneo ya mijini maambukizi ni asilimia 8.7 huku maeneo ya vijijini mambukizi yakiwa ni asilimia 4.7 wakati mkoa wa Mara ukiwa na aslimia hizo 7.7 na kuwataka washiri hao kutumia uwezo wao katika kuweka mikakati ya kupunguza kasi ya maambuzi ya ukimwi.
“Ndugu washiriki na wadau wa mkoa wa Mara tutambue kuwa hali ya ukimwi hapa mkoani imekuwa ikipanda kila kukicha sasa nazitaka afua na asasi nyingine zilizokatika mapambano dhidi ya ukimwi kuangalia kwa kina kinachochangia kasi ya maambukizi ya ukimwi mkoani kwetu kwani hali ilivyohivi sasa hapa kwetu inatisha”alisema RC Mfuru.  
Alisema ili kupunguza kasi hiyo ya maambukizi ya virusi vya ukimwi pia washiriki hao wanapaswa kuwa makini kwa kushirikisha jamii hususan makundi yaliopo katika mazingira hatarishi yanashiriki katika utekelezaji na ufanisi wa mkakati huo.
Hata hivyo RC Mfuru,alizionya asasi za kiraia ambazo zimekuwa zikitumia misada ya wafadhili kwa mgongo wa kutoa elimu na kuhudumia kwa jamii hususani kwa watoto yatima na wagonjwa majumbani na kwamba amesema mkoa wake hautasita kuchukua hatua kwa asasi hizo.
Kwa upande wake mmoja ya wawezeshaji wa asasi ya St Associate inayoratibu warsha hiyo Patrick Kanyamwenge,alisema lengo la mpango huo ni kupunguza maambukizi kwa asilimia 25 ifikapo mwisho wa mwaka 2012.
Warsha hiyo ya kupanga mipango ya mkoa na halmshauri ya kupunguza maambukizi ya VVU imeandaliwa na shirika la kitaifa la kuhudumia watoto UNICEF kupitia kwa tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi TACAIDS na kuratibiwa na shirika moja lisilo la kiserikali la ST Associates.

No comments:

Post a Comment