Saturday, February 26, 2011

CHADEMA KUUNGURUMA LEO MUSOMA

Musoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo kinatarajia kufanya maandamano makubwa katika Manispaa ya Musoma kwa kushirikisha viongozi wa juu wa chama hicho ambayo yataitimishwa na mkutano utakaofanyikia viwanja vya shule ya msingi ya Mkendo.

 
Maandamano hayo pamoja na kushirikisha karibu wabunge wote wa chama hicho pia yataongozwa na viongozi wa juu wakimwemo mwenyekiti wa taifa Freeman Mbowe na katibu mkuu wake Dk Wilbrod Slaa.

 
Mkurugenzi wa idara ya Utafiti na Sera taifa ambaye ni mratibu wa maandamano na shughuli zote za mikutano mkoani Mara Mwita Mwikwabe Waitara,aliliambia Nipashe jana kuwa tayari polisi wabariki kufanyika kwa maandamano hayo ya amani na mikutano katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara.

 
“Jana (juzi) katika kikao chetu na kamanda wa polisi wa mkoa(RPC)mkuu wa polisi wa wilaya(OCD)na mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU mkoa tulikubaliana njia za kupita maandamano hayo kwanza yatapolelea eneo la Bwiri,kasha kupita barabara ya Nyerere,Shabani,Mkendo,Kusaga na kurudi barabara ya Nyerere na kuingia uwanja wa Mkendo”alisema Waitara.
Aidha Waitara aliwaomba wananchi kuwasili katika eneo la Bweri kimlometa nane kutoka mjini hapa majira ya saa 3 kamili ambapo alisema maandano hayo yanatarajia kuanza kuanzia saa tano kabla ya kuitishwa kwa mktano huo katika uwanja wa Mkendo ambao utahutubiwa viongozi mbalimbali wa chama hicho.

 
Alisema miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kuhusu kupinga serikali kuilipa shilingi bilioni 94 kampuni ya kufua umeme ya Dowans,kuzungumzia uchaguzi wa Meya wa arusha ambao ulisababisha kutokea kwa mauji,kuitaka serikali kudhibiti mfumuko wa bei katika bidhaa mbalimbali nchini suala la kuandikwa kwa katiba mpya.

 
Hata hivyo Waitara alisema baada ya mkutano huo leo,kesho feb 27 viongozi hao wa chadema watagawanyika katika makundi sita kwaajili ya kufanya mikutano kama huo katika majimbo yote ya uchaguzi ya mkoa wa Mara.

 
Alisema awali chadema iliomba pamoja na njia hizo pia kutumia njia za Nyasho,Majita road na Uhamiaji lakini walishauriana na polisi kusitisha njia hizo tatu kutokana na ufinyu wa barabara ili kuondoa msongamano kwa wananchi wengine.

 
Alisema februari 28 hadi machi mosi mikutano na maandamano kama hayo itafanyika mkoani Shinyanga na Machi tatu wanatarajia kuwa mkoani Kagera katika kuhitisha mikoa ya kanda ya ziwa kabla ya kupanga mikoa mingine.

 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara kamishina msaidizi Robet Boaz,alisema jeshi la polisi limeruhusu kufanyika kwa maandamano hayo ya amani na mikutano hiyo.

Mwisho

No comments:

Post a Comment