Tuesday, January 11, 2011

JAMII YA WAMASAI NGORONGORO WAHITAJI SHULE

 
JAMII ya kimasai inayoishi katika hifadhi ya Ngorongoro bado ina matatizo makubwa katika suala zima la elimu hasa ikizingatiwa serikali inasema kuwa tayari imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga shule kila kata ambapo mtoto wa kitanzania hatokaa nyumbani wkwa kukosa shule
 
Katika uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa gazeti hili aliyekuwepo katika hifadhi hiyo imegundulika kuwa pamoja na serikali kutoa takwimu nzuri zinazoonyesha kufanikiwa katika sekta za elimu lakini bado jamii hiyo inaonekana kusahaulika mpka kufikia na kusema kuwa pengine wao si watanzania.

 
 
Ndani ya eneo hilo la Ngorongoro kuna boma amabalo hutumiwa na jamii ya wamasai ambao wameungana kutoka katika vijiji vya Endure,Esele na Olpiryo ambapo watoto wa jamii hiyo wameonekana kuhitaji elimu lakini kikwazo kimekuwa ni majenngo pamoja na walimu ambao watawatoa katika wimbi la watu wasiokuwa na elimu
 
Akiongea katika eneo hilo la Boma mwalimu aliyejitolea kuwafundisha wanafunzi hao wa shule ya awali ya Kiroki Mwalimu Paul Demlwa alisema kuwa serikali imewasahau kitu ambacho kinapelekea watoto wa jamii hiyo kukosa elimu kama inavyortakiwa

 
 
Mwalimu huyo ambaye ni mhitimu wa stashahada katika chuo cha Butimba jijini Mwanza ambapo alisema kuwa hakupenda kuajiriwa katika shule za mjini ambapo shule ni nyingi nakuacha jamii yake ya kimasai ikikosa elimu wakati yeye anaweza kuwa mwanga katika jamii hiyo.
 
  ‘Mimi nimemaliza katika chuo cha Butimba jijini Mwanza lakini sikupenda kuajiriwa wakati jamii yangu ya kimasai inakosa elimu “ alisema mwalimu Paul katika Kiswahili chenye lafudhi ya kimasai
 
Alisema shule ambayo pengine vijana hao wangesoma katika kupata elimu japo ya msingi ipo mbali kilomita 36 kitu ambacho hakiwezekani kwa kijana kwenda na kurudi ikizingatiwa hata shule hizo hakuna chakula  ambacho mwanafunzi angeweza kula huko.


 
 
Mbali na kusema hivyo Mwalimu Paul alisema kuwa waliamua kuishi katika eneo hilo kwani ni eneo ambalo ndio njia inayopitiwa na watalii ambao kwao ni njia rahisi ya kupata fedha tofauti na watakapo kwenda kuishi mbali kwani kazi za mikono yao ndio uwaingizia fedha na ikizingatiwa wageni wanapenda kujua historia ya jamii hiyo.
 
Aidha baadhi ya wamasai katika eneo hilo walisema kuwa hakupenda kuishi katika ameneo hayo bali ugumu wa maisha ndio chanzo cha wao kwemnda kuishi ndani ya hifadhi hiyo.
 
    “Sio kwamba sisi tunapenda kuishi katika bonde hilo bali ugumu wa maisha ndio unasababisha twende huku maana hatuna pesa na maisha yanazidi kuwa magumu”walisema wamasai hao
 
Walisema kuwa wanashukuru uongozi wa hifadhi ya Ngorongoro kwa msaada mkubwa wanaowapatia kwani bila kufanya hivyo pengine hawajui wangeishi vp hasa kipindi ambacho watalii hakuna.
 
Waliongeza kuwa kinachotakiwa kwasasa ni uongozi wa hifadhi hiyo kuongeza japo fungu ambalo litasaidia katika mahitaji yao kulingana na hali ya sasa ya maisha hasa katia suala ziama la matibabu.


 
 
Akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro mkuu wa hifadhi hiyo Bernad Murunya alisema kuwa wamekuwa na mahusiano mazuri na jamii ya wafugaji ambao wamekuwepo eneo hilo tangua zamani kitu ambacho kitasababisha huduma kwa jamii hiyo liwe ni jambo la msingi.
 
Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1959 wenyeji wa eneo hilo wameongezeka kutoka watu elfu 8000 mpaka kufikia watu elfu 64000 lakini pamoja na wingi huo bado hifadhi hiyo inajitahidi kuwaendeleza kwa kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya jamii hiyo.


 
Mrunya aliongeza kuwa bajeti hio ni pamoja na kusaidia mifugo yao katika kuwapatia chanzo,kujenga mabwawa,kuwapa maji,kujenga miundombinuna kama barabara, ulinzi na elimu kama kujenga shule katika maeneo ya jamii jiyo ya kimasai.



Alisema kwa sasa wanaangalia jinsi ya kuboresha sekta ya elimu katika jamii hiyo ingawa tayari waliishaanza kusomesha vijana kutoka shule za msingi mpaka vyuo vya kati,aliongeza kuwa mwaka uliopita walisomesha vijana 1048 kutoka msingi mpaka chuo kikuu ambapo wanamuongozo wa kuwasaidia wale wasiojiweza.
 

No comments:

Post a Comment