Hizo ni picha mbalimbali zinazoonyesha kituo kikuu cha mabasi mjini Musoma
Tangu mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amezindua kituo kikuu cha mabasi mjini Musoma hata mwaka miaka miwili bado hajaisha lakini tunashuhudia jinsi kituo hicho kilivyoanza kubomoka kuna maswali mengi ambayo kupata majibu yake unaweza kumaliza miaka kibao
Je ina maana viongozi wa Serikali hasa katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma hawaoni kinachotokea katika kituo hicho au wanafumbiana macho? nani alipitisha kujengwa kwa kituo hicho kikuu cha mabasi mjini Musoma sehemu ambayo inatwamisha maji? Mdau nilijaribu kutafuta majibu ya maswali haya kwa uchache bado sijapata lakini nakuahaidi nitakueleza pale yatakapokamilika
No comments:
Post a Comment