Friday, December 3, 2010

SAMAKI KATIKA SOKO LA KWASANANE

 Watu wa mkoa wa Mara wanaaminika kwa ufikirivu wao ulivyo wa hali ya juu lakini pamoja na kuaminika hivyo wengi huwa hawajui nini kinachosababisha,ndugu yangu ni wingi wa samaki kama hawa wanaopatikana ziwa Victoria ingawa wavuvi wanavua mpaka samaki wadogo lakini elewa chanzo ni samaki hawa.


                                                        AJIRA JAMANI HADI USIKU

Mtoto huyu ambaye hakufamika kwa jina mara moja alikutwa na kamera ya Mwana wa Afrika katika mtaa wa Mukendo usiku akiuza ndizi na maembe na nilipomdadisi alisema kuwa ametumwa na mama yake ili apate fedha ya kununua sabuni.kuhusu shule alisema kwa sasa ni mwezi wa pili haendi shule kisa hana fedha za kununua nguo. Nilimuahidi nitamsaidia katika suala la nguo(jamani kutoa ni moyo)

No comments:

Post a Comment