Thursday, October 14, 2010

UJUMBE WA NGU OKTOBA 14 (NYERERE DAY)

Sisi watanzania tunafahamika kama kisiwa cha amani duniani kitu ambacho msingi wake umewekwa na mwasisi wa Taifa hili Hayati Julius Kambarage Nyerere,Leo tunakumbuka miaka 11 tangu mzee wetu aondoke duniani nini tunajifunza kupitia hotuba zake?

Ni aibu kubwa leo tukafanya uchaguzi huku tukiwa na makovu ya mapanga eti sababu tumepigana sababu ya ushabiki wa vyama vya siasa,hilo ni doa kubwa katika taifa letu.

Njia pekee ya kumuenzi Mwalimu ni kudumisha amani,upendo na mshikamano kama alivyotufundisha toka zamani bila kusahau kuepuka udini,ukabila na ubaguzi wa rangi au kitu chochote.

                                                                                                                       Na Augustine Mgendi
                                                                                                    

No comments:

Post a Comment