Tuesday, September 28, 2010

WAANDISHI WA HABARI MARA WAMSUSIA RC

MUSOMA
BAADHI ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari manispaa ya Musoma mkoani Mara jana walisusia mwaliko wa mkuu wa mkoa huo kanali mstaafu Enos Mfuru kwa kile kilichodaiwa mkuu huyo kubagua vyombo vya habari.
Taarifa zinasema kuwa mkuu wa mkoa huyo aliwaalika wanahabari ili aweze kuongea nao kuhusu uzinduzi wa siku ya maziwa shuleni ambapo kitaifa itafanyika manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Wakiongea kwa jazba baada ya kupigiwa simu na Jumanne Mwasamila ambaye ni afisa mshauri wa maeneleo ya jamii mkoa wa Mara juu ya mwaliko huo wa mkuu wa mkoa,walisema kuwa wamechoshwa kutumika kama kondom kwani mkuu huyo anapokuwa na shida kubwa ndio uona vyombo vya habari vya taasisi zingine vina umuhimu.
Walisema kuwa mkuu huyo amekuwa akiona chombo cha habari cha serikali (TBC) na Chama cha Mapinduzi ( Gazeti la Uhuru) kuwa ndio vyombo pekee ambavyo vinaweza kufanya kazi zake katika uwafikia wananchi
  “Mkuu sisi tunakuheshimu sana lakini kwa mwaliko huo wa mkuu wa mkoa hatutaki maana sisi tunaonekana kama kondom kwanini mtu anakuwa na thamani pale tu mhusika anapokuwa na shida yeye atafute hao hao ambao siku zote hufanya nao kazi” alisema George Marato mwandishi habari wa ITV na Radio one

                               
Marato aliongeza kuwa hivi karibuni kulikuwa na mbio za mwenge mkoani hapa lakini walipokwenda ofisi ya mkuu wa mkoa walikuta vyombo vingine vya habari havina mwaliko ila ni TBC na gazeti la Uhuru huku Radio ya mkoani hapa Victoria Fm ikipewa nafasi mwisho kwa kuwa inapatikana mjini hapa.
Mbali na tukio hilo pia waandishi hao walisema kuwa kumekuwa na matukio mengi ambayo mkuu huyo amekuwa akionyesha ubaguzi wa wazi kwa vyombo vya habari mfano ni siku alipokwenda kukagua barabara ya Serengeti ambapo alisema kuwa anahitaji TBC kwa kuwa ndio chombo ambacho kinaweza kuandika.
Pia hali kama hiyo imekuwa ikijitokeza katika ziara za viongozi mbalimbali wanaokuja mkoani hapa ambapo hata kama kuna gari ambayo itahitajiwa na waandishi wa habari lazima mtu wa TBC awepo ndipo chombo hicho kiweze kutolewa.
Matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara mkoani hapa ingawa sasa imefika wakati na waandishi wa habari kugoma kufanya kazi za mkuu huyo wa mkoa mpaka pale atakapokubali kufanya kazi na vyombo vyote vya habari katika mji wa Musoma.
Wakati huo huo waandishi wa habari mjini hapa jana wamekata mzizi wa fitina baada ya kumweleza kamanda wa Polisi mkoani Mara kamishina msaidizi Robert Boaz kuwa kumekuwa na ushirikiano hafifu kwa Afisa mnadhimu wa jeshi la Polisi mkaoni hapa Mambo Masige ambaye huachiwa ofisi na kamanda huyo anapotoka.
Waandishi hao walimweleza kamanda Boaz kuwa pengine kuna taarifa ambazo wamezisikia lakini lazima waende polisi ili wahakikishe lakini wanapofika katika ofisi ya mkuu huyo hushindwa kuonyesha ushirikiano na wana habari hao.
 ‘Kamanda tunaomba unapotoka umwache mtu anayeweza kutupatia habari ambazo zitakuwepo au pengine tumezisikia maana afande Masige ameonyesha kutokuwa na ushirikiano na sisi` alisema Berdina Nyakeke mwandishi wa gazeti la The Citizen.
Aidha kufuatia tuhuma hizo kamanda Boaz alimwita afisa huyo na kutaka waandishi hao kueleza tena ili nae asikie ambapo afisa huyo wa jeshi la polisi alisema kuwa wakati mwingine wanandishi hao wa habari wanafika wakiwa wanahitaji habari ambazo zingine bado hazijakamilika kitu ambacho si kweli.
Kufuatia sakata hilo Afisa mnadhimu huyo wa jeshi la Polisi alihaidi kufanya kazi vizuri na waandishi wa habari kwani taasisi hizo hutegemeana katika sekta ya kupasha na habari

No comments:

Post a Comment