Monday, August 23, 2010

WATANZANIA TUIPENDE NCHI YETU

Watanzania habari za mihangaiko kwa siku ya leo bila shaka bado ni pilikapilika za kampeni katika chaguzi zinazotukabaili hapo oktoba mwaka huu yaani uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani.Ni kitu kizuri kwani ndio utaratibu wa nchi yetu katika nyanja nzima za demokrasia.

Pamoja na kuwepo kwa mchakato huo watanzania ni bora kwanza kutakatunguliza masilahi ya nchi yetu kuliko masilahi ya mtu binafsi kwani kwa kufanya hivyo wale wanyonge hawatakuwa na chao mbele ya walichonacho,wanapenda kuwatumia wenzao katika kutafuta madaraka lakini pale wanapofanikiwa ndio mwisho wa kuonekana katika majimbo yao.

Mtanzania kama kuna sehemu ambayo itabidi uwe makini basi ni katika uchaguzi huu kwani kuna maneno matamu sana kutoka kwa wagombea mpaka kufikia wengine kusalimia watoto wadogo jamani katika hilounahitaji kukuna kichwa upate jibu?

Hongera sana kwa wabunge ambao tayari inasemekana hawana mpinzani katika majimbo yao kutokana na wengine kushindwa gharama za uchaguzi na wengine kukubali utendaji wa mbunge anayegombea au kutetea nafasi yake katika jimbo huska,kitendo hicho kwangu naona ni kama kuheshimu mchango wa mtu huska alioufanya katika jimbo hilo.

Kuna wabunge wengi ambao tayari taarifa zinasema kuwa wasimamizi wa uchaguzi wamewatangaza kama wabunge wateule akiwemo mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Nimroad Mkono,Masha,Ngereja na wengine kibao Mungu awe nanyi.

  Ipende nchi yako kama upendavyo nafsi yako 

             MUNGU IBARIKI TANZANIA

No comments:

Post a Comment