Serikali imewataka Wajasiriamali wadogo kuwa na Mkakati wa
Pamoja katika kuhakikisha bidhaa mbalimbali za Tanzania zilizoongezwa thamani zinauzwa
nje ya nchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Kazi na Ajira Bi
Gaudencia Kabaka katika ufunguzi wa Maonyesho ya Kanda ya Ziwa ya Viwanda
vidogo vidogo Sido kwa Mwaka 2013 katika
viwanja vya shule ya Msingi Mkendo manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Bi
Gaudencia Kabaka- Waziri wa Kazi na Ajira
Alisema kitendo cha kupeleka Malighafi nje ya nchi husababisha
kukosekana kwa ajira hapa nchini na hivyo kuwataka wafanyabiashra wadogo kuweka
mkakati wa pamoja kuuza bidhaa nje ya Tanzania na si Malighafi.
" Tushirikiane kwa pamoja katika kuhakikisha bidhaa zetu zinauzwa nje ya nchi na si tupeleke Malighafi maana tunapeleka na ajira za watu" alisema Waziri Kabaka
Waziri kabaka akikagua banda la Sido
Katika hatua nyingne Waziri Kabaka aliwaomba wakuu wa
Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwatambua WajasiriaMali katika
Maeneo yao,
kuwaongezea ubunifu na kuwatengea Maeneo ya kufanyia shughuli zao.
Awali akimkaribisha Waziri Kabaka,Kaimu Mkurugenzi wa Sido
Bw Pius Wenga aalisema bidhaa za Tanzania
zilizopo katika Maduka na Supermarket bado ni chache ikilinganishwa na nchi
jirani.
Mapema katika ufunguzi huo Wazir kabaka alikagua mabanda
mbalimbali katika Maonyesho hayo ya Kanda ya Ziwa ya Sido ambayo yameelezwa ni ya tatu kufanyika Mkoani Mara ambapo
yalifanyika kwa Mara ya Kwanza mwaka
2004,2008 na 2013.
Waziri kabaka katika Picha tofauti
No comments:
Post a Comment