Mamlaka ya Chakula na Dawa kanda ya Ziwa TFDA kwa kushirikiana na uongozi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara umeteketeza bidhaa mbalimbali zisizofaa kwa Matumizi ya binadamu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9.
Mkaguzi wa dawa kutoka ofisi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa kanda ya Ziwa TFDA Bw Agrey Mwambuki alisema katika zoezi hilo walifanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali kama vipodozi,dawa na vyakula visivyofaa kwa Matumizi ya binadamu
Bw Mwambuki alisema kuwa zoezi la kukamata na kuteketeza bidhaa zisizofaa litakuwa endelevu kwa Manispaa ya Musoma huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanatumia bidhaa salama kwa kuhakiki maelezo yaliyopo katika bidhaa huska.
“Zoezi hili ni endelevu kwa Manispaa ya Musoma nah ii ni kutokana na bidhaa nyingi kutokidhi viwango na hivyo kuweza kuhatarisha Afya za watumiaji” alisema Bw Mwambuki
Zoezi la kuteketeza bidhaa hizo zilizokuwa na tani moja na nusu ziliteketezwa katika eneo la Nyambange nje kidogo ya Manispaa ya Musoma
Bw Agrey Mwambuki-Mkaguzi wa dawa kutoka ofisi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa kanda ya Ziwa TFD
Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa Manispaa ya Musoma Dr Kitwala Makwi alisema bidhaa zisizofaa kwa Matumizi ya Bindamu huwa athari kubwa katika ngozi,figo na hata kusababisha kansa na hivyo kuwataka wananchi kuwa Makini wanaponunua bidhaa hizo
“Kila bidhaa huwa zimeandikwa viambata vinavyofaa lakini pia watumiaji waangalie tarehe zinazoonyesha mwisho wa Matumizi ya bidhaa huska” alisema Dr Kitwala Makwi.
Dr Kitwala Makwi.-Kaimu Mganga mkuu wa Manispaa ya Musoma
Baadhi ya bidhaa zisizofaa kwa Matumizi ya binadamu zikiteketea
Katika hatua nyingne Bw Cprian Bartazar ambaye ni mmoja wa waathirika na kamatakamata hiyo aliwaasa wafanyabiashara na watumiaji wa bidhaa mbalimbali kupata ushauri kabla ya kutumia ikiwa ni njia ya kulinda Afya zao.
Zoezi hilo lilielezwa litakuwa endelevu kwa Manispaa ya Musoma hapa pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi kubaini bidhaa visivyofaa kwa Matumizi ya binadamu.
No comments:
Post a Comment