KISU KINACHODAIWA KILITUMIKA KUMUUA BODA BODA
MAITI IKIWASILI HOSPITALI YA WILAYA SERENGETI
Oktoba 25,2013
MTU mmoja anayetuhumiwa kuhusika
na mauaji ya aliyekuwa boda boda mjini Mugumu Wilayani Serengeti Gwitembe Yagera(60)amekamatwa
na kudai kuwa aliambiwa na Sangoma wake aue mtu yeyote ili apate utajiri.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara
Fernandi Mtui alithibitisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa huyo anayeshikiliwa na
polisi wilayani Serengeti Elias Jonathan(23)mkazi wa kijiji cha Burunga kata ya
Uwanja wa Ndege wilayani hapa,amekamatwa hivi karibuni eneo la Sirari na kuwa
uchunguzi zaidi unaendelea .
Habari kutoka ndani ya jeshi la
polisi zinadai kuwa mtuhumiwa huyo alisema kuwa alitekeleza mauaji hayo
kutokana na masharti ya mganga wake ambaye anasakwa na jeshi la polisi,kuwa
afanye mauaji pekee yake na kwa mtu yeyote ndipo na atapata utajiri.
“Alisema aliamua kumkodi huyo
boda boda kwa kuangalia umri wake kwa madai kuwa anakwenda Mosongo…kufika eneo
la Nyisense Nyichoka akamchoma kisu na kusababisha mauaji yake na kukimbia
akitelekeza kisu hapo na hakuchukua kitu chochote”kilisema chanzo cha uhakika
kutoka ndani ya jeshi la polisi.
Kuhusu kukamatwa kwake chanzo hicho kilisema baada ya kutenda unyama
huo alitoroka hadi Sirari na ambako alihusika katika mauaji ya baiskeli na
kukamatwa ,na baba yake alitoa ushirikiano baada ya kujua kuwa anatafutwa kwa
mauaji na kunaswa na kuletwa Mugumu kuhusiana na tuhuma hizo.
Oktoba 4,mwaka huu majira ya saa
8 arasili mtuhumiwa huyo anadaiwa alimkodi Yagera kwa sharti kuwa wakifika
kijijini Mosongo angemlipa fedha yake,lakini kabla ya kufika inadaiwa alimchoma
kisu eneo la kushoto chini ya ubavu na kusababisha kifo chake.
Na baada ya kutenda unyama huo
hakuchukua kitu na kutokea na maiti yake iligunduliwa na wapiti njia ambao
walitumia simu ya marehemu kuwataarifu viongozi wa chama cha waendesha pikipiki
wilayani hapo,na askari polisi.
Habari tulizozipata wakati
tunaandaa taarifa hizi zinadai kuwa mtuhumiwa huyo amefikishwa katika mahakama
ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti kuhusiana na tuhuma hizo,hata
hivyo hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza
kesi za mauaji.
No comments:
Post a Comment