Wednesday, November 13, 2013

WAFANYABISHARA WAHIMIZWA KULIPA KODI KWA HIARI

 Juu Meneja wa TRA Mara Bw Joseph Kalinga akisoma taarifa katika kilele cha wiki ya Mlipa kodi
 Baadhi ya Wafanyakazi wa TRA MARA
 Mkuu wa wilaya ya Musoma Bw Jackson Msome
 Nahodha wa TRA MARA akipokea Kombe baada ya ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wafanyabiashara FC
 MUSOMA

Serikali Mkoani Mara imewahiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari ikiwa ni Mikakati ya kusukuma mbele maendeleo ya Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa alitoa kauli hiyo katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Musoma Bw Jackson Msome katika Maadhimisho ya wiki ya Mlipa kodi yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.


" Ni vyema wafanyabiashra wakajenga tabia ya kulipa kodi kwa hiari lakini pia kwa wakati kwani kodi hizo ndizo zinafanya barabara zinajengwa,madawa yanaptikana,shule zinajengwa na mambo mengine"alisema Mkuu wa wilaya hiyo

Alisema kulipa kodi kwa hiari ni jambo jema na la kizalendo ambalo husaidia kuleta Maaendeleo katika Taifa kwani kushindwa kulipa kodi husababisha kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa huku akikemea baadhi ya watumishi TRA wasiokuwa waaminifu.

 
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kwasasa baadhi ya Maafisa wa TRA wamekuwa si waaminifu katika kazi zao ambapo husababisha wnanchi kutokuwa na Imani nao.

Kwa Upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoani Mara Bw Joseph Kalinga aliwashukuru baadhi ya wafanyabiashara wanaotimiza wajibu wao katika kulipa kodi huku akisema TRA Mara kwa Mwaka wa fedha 2012/2013 ulivuka lengo la ukusanyaji kodi lililokuwa limewekwa. 


" Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Wafanyabiashara wote ambao wamekuwa wakilipa kodi kwa wakati ambapo husababisha Mkoa wetu kuvuka Malengo" alisema Meneja wa TRA







Katika maadhimisho hayo ya Saba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA yalitanguliwa na Maandamano katika Maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara kabla ya kuhitimishwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo Mjini hapa.

No comments:

Post a Comment