|
Mkurugenzi
wa Mwananchi Communications Tido Muhando (kulia) akimkabidhi tuzu
Absolom Kibanda mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya
Uandishi wa Kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi |
MHARIRI Mtendaji wa
New Habari 2006 Ltd. Absalom Kibanda ameibuka mshindiwaTUZO ya uandishi
wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi iliyoandaliwa na
Muungano wa Klabu za waandishi wa Habari nchini (UTPC) na kujipatia
kiasi cha shilingi milioni 10.
Kibanda
alitangazwa leo Jijini Mwanza na Jopo la Majaji walioteuliwa kufanya
mchakato wa kumtafuta mwaandishi wa Habari bora kwa mwaka huu kwenye
hafla fupi katika Hoteli ya JB Belamont na kuhudhuliwa na Wahariri wa
Vyombo vya Habari, viongozi wa UTPC,Viongozi wa Klabu za Waandishi wa
Habari nchini , Wanahabari na Wageni mbalimbali zaidi ya 120 kutoka
ndani na nje ya Tanzania'
|
Kibanda
akinyanya juu Tuzo kuonyesha wadau na wageni waalikwa ikiwa ni ishara
ya ushindi kushoto ni Rais wa UTPC Keneth Simbaya na kushoto ni
Mkurugenzi wa Mwananchi Communications Tido Muhando. |
|
Kibanda akifuta machozi kwa kutoamini kama ndiye amekuwa mshindi wa Tuzo hiyo. |
|
Leila Sheikh ambaye alikuwa moja kati ya majaji akimtuliza Kibanda baada ya kumtangaza kuwa mshindi wa Tuzo. |
|
Huyu alishindwa kabisa kujizuia. |
|
Wageni mbalimbali wamehudhuria tukio hili la kwanza kabisa katika historia ya habari nchini Tanzania. |
|
Wanahabari wakipeperusha taarifa. |
|
Kwa umakiiiiini...! |
Mjumbe wa Kamati ya
Majaji hao Hamza Kassongo kwa idhini ya Mwenyekiti wake Nkwabi
Mwanakilala alisema kwamba Jopo la Majaji lilitembea Mikoa mbalimbali
nchini kupita na kufanya utafiti kwa waandishi wa habari na wahariri
wanaotekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi na kupambana na vitendo vya
udhalilishaji na unyanyasaji kutoka kwa viongozi wa serikali, wanasiasa
na makundi mbalimbali ikiwa ni lengo la kuwatisha waandishi hao.
Kassongo
aliwataja majaji wengine wanne ambao walitumia muda kufanya uchambuzi
wa kumpata mshindi kuwa ni pamoja na Nkwabi Mwanakilala (Mwenyekiti),
Hamza Kassongo, Leila Sheikh, Dr. Ayoub Ryoba na Rosemary
Mwakitwange(wote wakiwa wajumbe wa jopo la majaji ambao wametekeleza
majukumu yao baada ya kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi wa UTPC kufanya
kazi hiyo kwa uadilifu na kufuata vigezo vilivyowekwa.
Msemaji wa jopo hilo la Majaji hao
aliongeza kuwa mshindi wa Tuzo hiyo ambaye ametangazwa amekidhi vigezo
na hakuna uchakachuaji na wakubaliane na uamuzi wa jopo hilo na kisha
alimwomba Leila Sheikh kupita mbele kumtangaza mshindi wa Tuzo hiyo
ambapo alimtangaza Kibanda kuwa mshindi wa waandishi wa habari nchini
kwa mwaka huu baada ya kushinda vigezo kumi viliyoainishwa..
|
Sambamba
na Tuzo pia mtunukiwa ametwaa kitita cha shilingi milioni 10 ambapo kwa
mujibu wake alitamka bayana kutoa nusu ya kiasi hicho kuchangia malezi
ya mjane wa marehemu Mwangosi na elimu kwa watoto wa marehemu. |
|
Absolom
Kibanda akihutubia baada ya kutangazwa huku Mkurugenzi wa UTPC Abubakar
Karsan akimsikiliza kwenye Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmonte Jijini
Mwanza. |
Mgeni rasmi wakati wa
Utoaji Tuzo hiyo, Tido Mhando alisema kwamba wanahabari sasa umefika
wakati wa kukataa kutumiwa na wanasiasa na viongozi mbalimbali wa
serikali na wafanyabiashara kwa kukubali kupokea fedha na bahasha jambo
ambalo ni hatari kwa wanahabari pamoja na kuwadhalilisha wanahabari kwa
madai ya kununuliwa na hata pengine ni kuidhalilisha taaluma nyeti
inayotegemewa na jamii kupata ukweli.
“Wananchi
wanatutegemea kuibua mambo mengi ya ufisadi, rushwa, wizi na hata
ujangiri ikiwemo ya uhalifu na uhamiaji haramu kushika kasi ndani ya
nchi yetu na hivyo waandishi kuwa majasiri kuyafichua hayo kwa kuandika
ukweli na bila kupotosha umma ili jamaii inayotutegemea iweze kutuamini
na kutupa ushirikiano wa dhati katika kutekeleza majukumu yetu kwa
uhakika zaidi”alisema.
Aliongeza kuwa kauli
za wanasiasa zinazotolewa Bungeni na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa
serikali wakati huu wa kujadiliwa Muswada wa Sheria kwa Vyombo vya
Habari nchini ni dhahili kuwa lengo kubwa ni kwakandamiza waandishi wa
habari na uhuru wa vyombo vya habari nchini katika kutoa habari kwa
wananchi.
Tido alisema kuwa Tuzo
kama hii ya Daud Mwangosi Herooic Journalism Servanthood Exellence
Award ni juhudi za wanahabari wenyewe kujibu maovu haya wanayotendewa na
watu mbalimbali, UTPC wametuonyesha mfano na wajibu wetu leo hii,
tunachowajibika kufanya ni kuwaunga mkono ili tuzo hii iweze kuendelea
kila mwaka.
Source Gsengo
No comments:
Post a Comment